Jumamosi moja
Ursula Nafula
Wiehan de Jager
Kiswahili


Jumamosi moja, mama alisema, "Brenda, Maria na Lona, nendeni mcheze!"
Waliondoka mbio pamoja.
Waliondoka mbio pamoja.
Lona alisema, "Twendeni mtoni tukaogelee."
Brenda alijibu, "Mama alitukataza kuogelea mtoni."
Brenda alijibu, "Mama alitukataza kuogelea mtoni."
Walifika mtoni wakavua viatu na nguo.
Wakacheza majini kwa muda.
Wakacheza majini kwa muda.
Walicheka na kushangilia.
Walifurahia maji baridi.
Walifurahia maji baridi.
Baadaye, Maria alisema, "Tuogelee zaidi. Mama hatajua."
Lona na Brenda walikubali wakaendelea kuogelea.
Lona na Brenda walikubali wakaendelea kuogelea.
Walipomaliza, hawakuziona nguo zao popote.
Walianza kuhisi baridi.
Walianza kuhisi baridi.
Hawakuzipata nguo zao popote.
"Tutamwambia mama nini?" Waliulizana.
"Tutamwambia mama nini?" Waliulizana.
Brenda alisema, "Lo! Ng'ombe anakula shati la Lona."
Lona alianza kulia.
Lona alianza kulia.
"Mwingine anakula sketi yangu!" Maria pia alilia.
Walisema, "Mama, ng'ombe walikula nguo zetu."
Hawakusahau adhabu aliyowapa.
Hawakusahau adhabu aliyowapa.
Maswali: 1.Taja majina ya watoto wote watatu tunaokutana nao katika hadithi hii. 2. Kwa mujibu wa Brenda, Mama aliwakataza watoto kufanya nini? 3. Watoto walihisije walipomaliza kuogelea? 4. Unafikiri watoto hawa walikuwa wamewahi kuogelea katika mto huo? Toa sababu kwa jibu lako. 5. Unafikiri watoto hawa walipewa adhabu gani?
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Jumamosi moja
Author - Nombulelo Thabane and Tessa Welch
Adaptation - Ursula Nafula
Illustration - Wiehan de Jager
Language - Kiswahili
Level - First sentences
Adaptation - Ursula Nafula
Illustration - Wiehan de Jager
Language - Kiswahili
Level - First sentences
© African Storybook Initiative, 2014 2014
Creative Commons: Attribution 4.0
Source www.africanstorybook.org
Creative Commons: Attribution 4.0
Source www.africanstorybook.org

