Jumamosi Alasiri
Nombulelo Thabane
Wiehan de Jager

Ilikuwa Jumamosi yenye joto jingi. Kila mtu alikuwa amenuna.

"Betty, Mercy na Larry, nendeni nje mcheze! Siwataki hapa," mama aliwaambia watoto.

1

"Twendeni mtoni. Kuna upepo mzuri huko." Larry alisema.

"Mama alitukataza kuogelea mtoni," Betty alijibu.

"Tutachezea tu karibu na maji," Larry alisema.

2

Walipofika, kwanza walivua viatu vyao. Lakini walikuwa bado wanahisi joto.

Wakavua nguo zao. Lakini walikuwa bado wanahisi joto.

3

Waliiweka miguu yao majini kuifanya iwe baridi.

Walirushiana maji. Punde kidogo walikuwa wameloa maji.

4

"Aa, njoo! Hebu tuogelee. Mama hatajua," Mercy alisema.

Waliogelea kwa muda mrefu wakasahau kuwa muda ulikuwa unapita.

5

Jua lilipoanza kutua, walihisi baridi.

Lakini je, nguo zao zilikuwa wapi?

6

Walitazama chini ya miti. Wakatazama juu ya vichaka.

Walitazama kila mahali. Hawakuona dalili ya nguo zao popote.

7

Ng'ombe walikuwa wakila nyasi karibu na mto.

Betty alisema, "Mwone yule ng'ombe! Ni nini hicho anachokula?"

"Anakula ua jekundu," Larry alisema.

8

"Sio ua jekundu. Ni shati lako." Mercy alipiga kelele.

Walimwona ng'ombe mwingine akila kitu cha kisamwati.

"Hiyo ni sketi yangu!" Betty alipiga kelele kwa hofu.

9

Walirudi nyumbani wakiwa wamevaa suruali tu. "Ng'ombe walikula nguo zetu," walilia.

Punde kidogo makalio yao yalikuwa na joto sana kwa kuadhibiwa.

10
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Jumamosi Alasiri
Author - Nombulelo Thabane, Tessa Welch
Translation - Brigid Simiyu
Illustration - Wiehan de Jager
Language - Kiswahili
Level - First sentences