Kobe na Kindi wanahitaji pesa.
Wanatengeneza sahani ili wauze sokoni.
Kobe anashuhudia vita sokoni.
Kindi na Fuko wanapigana.
"Mwache rafiki yangu," Kobe anapiga mayowe.
Fuko anamuuma Kobe kwenye pua.
Pua lake lililovunjika linaumia sana.
Kobe ana pua kombo kwa kuwa na haraka ya kupigana.