Watu hawa wana maoni tofauti.
"Walimu ni muhimu zaidi. Mnatuhitaji sisi kujifunza," mwalimu anasema.
"Wajenzi ni muhimu. Mnahitaji nyumba," mjenzi anasema.
“Seremala ni muhimu zaidi. Mnahitaji samani.”
"Madaktari ni muhimu zaidi. Mnahitaji matibabu."
"Wakulima ni muhimu zaidi. Mnatuhitaji kwa chakula."
"Wanafunzi ni muhimu zaidi!" Mwanafunzi anasema.
"Nyote mlikuwa wanafunzi kwanza!" Wote wanakubaliana.