Marafiki wawili wadogo
Belainesh Woubishet
Jesse Pietersen

Hapo zamani za kale, kulikuwa na Mbuzi Mdogo na Chui Mdogo.

Walikuwa marafiki.

1

Siku moja walienda kucheza pamoja uwanjani.

2

Walirudi nyumbani jioni sana.

3

Mbuzi Mdogo alimwambia mamake, "Nilikutana na rafiki mrembo. Ana madoadoa maridadi. Nimefurahi sana. Nitakutana naye tena kesho."

4

Mamake Mbuzi Mdogo alijibu, "Mwanangu, nimefurahi umerudi salama. Huyo si rafiki yetu. Sitakuruhusu ukutane naye tena."

5

Wakati huo huo, Chui Mdogo alimwambia mamake, "Nilikutana na rafiki mrembo. Anapenda kucheza sana. Nimefurahi. Nitakutana naye tena kesho."

6

Mamake alijibu, "Aa, maskini mwanangu. Huyo alikuwa mbuzi mdogo mrembo. Nasikitika hukumla. Utakapokutana naye kesho, muue na umle. Usiogope."

7

Siku iliyofuata, Chui Mdogo alienda katika kijiji cha Mbuzi Mdogo.

8

Hakumwona Mbuzi Mdogo pale nje.

Alikuwa amejificha nyumbani kwa mamake.

9

Chui Mdogo alipaza sauti, "Twende uwanjani tukacheze."

10

Mbuzi Mdogo alijibu, "Sisi si marafiki tena. Leo siji. Nimemsikiza mamangu. Mtoto mzuri humsikiza mamake."

11

Chui Mdogo alihuzunika.

Alirudi kwa mamake.

12
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Marafiki wawili wadogo
Author - Belainesh Woubishet
Translation - Susan Kavaya
Illustration - Jesse Pietersen
Language - Kiswahili
Level - First sentences