Haaaa! Nyumbani kwetu, kuna ng'ombe wa ajabu.
Ana pembe moja tu na hana mkia. Ni ng'ombe mzuri sana.
Ni ng'ombe mnono aliye na tumbo kubwa.
Ni ng'ombe aliye na nguvu.
Mchungaji anampenda ng'ombe huyu sana. Amemfunza kuitambua sauti yake pekee.
Ng'ombe huyu anapokuwa malishoni, hujitenga na ng'ombe wengine.
Ni ng'ombe aliye hodari katika vita. Ng'ombe wengine wanamwogopa.
Watu wengi wanamjua ng'ombe huyu. Wanamwogopa kwa sababu yeye hupigana kwa pembe yake moja. Je, ukikutana na ng'ombe wa aina hii, utafanyaje?