Nilisikia upepo.
Ulivuma na kupita kwa kasi karibu na makao yetu.
Upepo huo ulikuwa mkali.
Uliibandua tiara yangu kutoka mkononi.
Niliifuata tiara yangu.
Lakini, upepo huo mkali ulinisukuma mbali nayo.
Upepo huo uligeuka na kuwa dhoruba.
Dhoruba hiyo iliienua tiara yangu juu zaidi.
Dhoruba hiyo ya kutisha, ilinimeza mzima mzima!
Sikuweza kuona chochote wala kugusa chochote.
Niliikumbuka tiara yangu nzuri.
Ilikuwa wapi?
Labda ilikuwa imenaswa mtini.
Au labda, ilikuwa bado inapeperuka hewani.
Mwishowe, dhoruba hiyo kali ilipunguka.
Mimi nilikuwa bado ninazunguka.
Nilipotulia, nilitazama mahali nilipokuwa.
Nilijiuliza, "Upepo ule mkali umeanda wapi?"
Sikuiona tiara yangu nzuri popote.
Sikuusikia tena upepo ukivuma.
Labda siku iliyofuata, ningeipata tiara yangu nzuri.
La muhimu kwangu ilikuwa kwenda zangu nyumbani, mbali na upepo hatari.