Hapo kale, mfalme wa mwitu alikuwa Bwana Simba.
Aliwatuma wanyama kukomesha kelele zilizofanywa na vyura. Wanyama hao hawakufaulu.
Tembo alijitolea kukomesha kelele hizo. Aliwekwa nje kuwa mlinzi.
Usiku wa manane kelele ziliposikika, Tembo alianza kuwaua vyura. Alifanya hivyo siku iliyofuata.
Baadaye, Mfalme Simba alikuwa mwenye furaha. Tembo alikuwa amezikomesha kelele za vyura.
Baada ya mwezi mmoja, waliwaona wadudu wengi shambani mwao.
Mfalme Simba alimwuliza Tembo kuwaita vyura ili wale wadudu wale.
Tembo alijawa na hofu. Alikuwa amewaua vyura wote. Alisema, "Samahani, samahani, ni-li-waua wote!"
Mfalme Simba alimwambia Tembo, "Nilikutuma kukomesha kelele, wala sio kuwaua vyura." Tembo alifungwa gerezani kwa miaka mingi!
Mfalme aliwashauri wanyama wote, "Fuateni maagizo yangu kila wakati."