Ninampenda mwalimu wangu.
Yeye ni mrembo mno. Ni mwalimu mzuri. Ni mtu mwema na mwenye subira.
Alivyosuka nywele zake zinapendeza sana.
Amezipamba na shanga za rangirangi.
Shanga zake ni za rangi ya kijani, nyeupe, nyekundu, na manjano.
Mama, tafadhali nisuke nywele zangu ziwe kama za mwalimu wangu?
Ningekuwa na umri mkubwa, ningezipamba nywele zangu kwa shanga.
Nitakua sawa kabisa na mwalimu wangu!