Kwa nini Nita ananing'inia kichwa chini?
Roxana Bouwer
Sarah Bouwer

Nita ananing'inia kichwa chini, nywele zake ndefu zikitetemesha ardhi.

Miti, nyasi, kila kitu hakiko njia sahihi.

1

Miguu yake, inapenya angani. Navi, mvulana mdogo, anapita.

Anasema, "Nimekuona hapa hapo awali. Umepinduka kichwa chini tena! Kwa nini?"

2

Miguu ya Navi inaonekana kuogelea kidogo angani. Anajaribu kujificha nyuma ya nywele za Nita.

"Ni vigumu sana kuzungumza," Nita anamwambia. "Mimi si sawa. Sifai."

3

Navi anamshika Nita mkono. Anataka kumsaidia kuelewa.

Wanapanda mti hadi sehemu ambayo Navi hutumia kutazama. Kutoka hapa juu wanaweza kuona mengi.

4

Wanatua na kuwatazama watoto wakicheza hapa na pale.

5

Watoto hao si sawa hata kidogo.

Abe anaonekana mviringo.

6

Chi amepakwa madoa.

7

Lala ni mrefu zaidi ya kawaida yake.

8

Bambam amesisimuka na anataka kuwa huru.

9

Lulu anasoma kimya kimya.

10

Tazama nywele za Freya.

Zinaonekana kama zenye kichaa.

11

Na Sid huvaa miwani kila mahali.

12

Na mimi, mimi ni ngozi na mifupa tu. Na wewe ni wewe. Hauko peke yako. Unaona, kila mwanadamu ni wa ajabu. Hilo linakufanya uwe sawa, kama mimi.

Dunia hii ni kama mchezo mmoja mkubwa sana. Ili kucheza, hatuwezi sote kuwa sawa.

13

Nita anahisi vizuri, shukrani kwa Navi, rafiki mpya aliyempata.

Kuning'inia kichwa chini, hakukufurahisha hata kidogo. Sasa anacheza na kila mtu.

14
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Kwa nini Nita ananing'inia kichwa chini?
Author - Roxana Bouwer
Translation - Ursula Nafula
Illustration - Sarah Bouwer
Language - English
Level - Longer paragraphs