Ngoma ya Magezi
Hlekane Paulinah Baloyi

Magezi anaanza kupiga ngoma yake yenye raingi nyeusi na nyeupe.

1

Watoto wanakusanyika karibu naye.

Wanaimba pamoja na ngoma.

2

Wanaimba, "Masingita ameolewa na nani? Ameolewa na mwenzetu mmoja."

3

Wanawake wanacheza kufuatia sauti ya ngoma.

4

Wanaume wanajiviringisha sakafuni, wakiruka juu na chini.

5

Mudungwazi anazungusha macho yake na kufanya dansi yake ya kuchekesha.

6

Wazee wanapiga filimbi na kutikisa vichwa vyao kwa mlio wa ngoma.

7

Wanawake wanazungusha nyonga zao na kupiga vigelegele.

Wote wanafurahia ngoma ya Magezi.

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Ngoma ya Magezi
Author - Hlekane Paulinah Baloyi
Translation - Anne Kamau
Illustration -
Language - Kiswahili
Level - First sentences