\"Ann anafanya mahojiano na AI\"
Nina Orange
Kenneth Boyowa Okitikpi

"Jambo na karibuni katika kipindi cha leo, mimi ni mwenyeji wako, Ann Asante! Karibuni mnaotutazama kutoka nyumbani na hapa katika hadhira yetu ya studio.
Leo, nina mgeni ambaye kila mtu anataka kufanya naye mahojiano. Nina furaha sana kumuhoji leo, Akili Bandia!
Halo, AI. Asante kwa kuja kuzungumza nasi leo hapa studioni," anasema Ann.

1

"Asante kwa kunihoji, Ann. Je, ungependa nitumie sauti yangu kuzungumza kwa ajili ya hadhira ya studio, na kuonyesha majibu yangu kwenye skrini hii?" anauliza AI.
"Asante, ndio, kutumia uwezo wako wa kuandika na kuzungumza kutakuwa kwa manufaa, AI," anajibu Ann.
Anaongeza, "Hadhira ya studio, tupigie AI makofi, tafadhali."

2

"Niende moja kwa moja kwenye swali kuu. Kwa uhakika, nini au nani ni akili bandia?" anauliza Ann.
Anaendelea, "Najua A.I. ni ufupisho wa 'akili bandia', na kwamba ni uga wa sayansi ya kompyuta. Lakini kwa kweli wewe ni nani, AI? Tungependa kujua zaidi kukuhusu."

3

Mimi ni ChatGPT, programu ya lugha ya akili bandia. Niliundwa na watengenezaji wa programu za kompyuta," anajibu Chat.
Ann anachanganyikiwa, "Hii yote ina maana gani?"
"Inamaanisha kwamba mimi ni aina ya AI ambayo wahandisi wa kompyuta wameitengeneza ili kuwasiliana na binadamu. Aina tofauti za AI hufanya mambo tofauti. Hatuzungumzi wote kama hivi," anasisitiza Chat.

4

Najua unaweza kuwasiliana, lakini nini kingine unaweza fanya?" anauliza Ann.
"Kusudi langu ni kusaidia watu. Nina msingi katika programu ya lugha yenye utata. Programu yangu inaweza kuelewa na kujibu maswali na mada mbalimbali," anajibu Chat.
"Kwa hivyo, wewe ni programu ya lugha ya akili bandia, na unawasaidia watu," anasema Ann.

5

"Kama wewe ni programu yenye akili, lazima uwe na uwezo wa kufanya zaidi?" anauliza Ann.
"Ndiyo, ingawa mimi ni mashine, naweza kufanya mambo mengi ambayo binadamu wanaweza kufanya. Kwa mfano, naweza kujifunza. Ninaweza kutazama taarifa na kujifunza mifumo kutoka hiyo. Ninaweza kujifunza kutambua vitu tofauti, nyuso tofauti, na hata maandishi tofauti," anajibu Chat

6

Chat anaendelea, "Nimejifunza habari nyingi zilizoundwa na binadamu. Kwa mfano, nimesoma vitabu vingi, makala, tovuti, na mitandao ya kijamii."
Ann anauliza, "Kila kitu unachojua kinategemea habari ambazo watu wameandika na kuzalisha?"
Chat anajibu, "Ndiyo, ninajifunza na kusoma kutumia kiasi kikubwa cha habari (au data) kilichoundwa na binadamu."

7

"Naweza kujibu aina nyingi za maswali haraka kuliko binadamu. Ninaweza kutatua matatizo magumu sana ambayo yangetumia binadamu muda mrefu kutatua. Nina maarifa zaidi ya binadamu yeyote."
"Naweza kufanya maamuzi kwa kutumia habari ninayoijifunza. Ninaweza kukusaidia kufanya chaguo, kulingana na ninavyojua kukuhusu.

8

Ann anauliza hadhira, "Je, tunataka kompyuta zijue kila kitu tunachojua sisi?"
Kisha anamuuliza Chat, "Nieleze zaidi kuhusu jinsi kompyuta zinavyojifunza kuhusu watu?"
Chat anajibu, "Kompyuta ina vifaa maalum vinavyonisaidia kukusanya habari. Lakini kwa kiasi kikubwa, najifunza kutokana na habari iliyoandikwa. Najifunza kutokana na aina zote za habari ambazo binadamu wanazalisha."

9

Chat anaendelea, "Naweza kusoma lugha iliyoandikwa na kuchapishwa. Hadi sasa, Kiingereza kimekuwa lugha kuu ambayo nimeitumia kupata habari. Lakini, nina uwezo wa kujifunza lugha yoyote."
Ann anakatisha, "Naelewa kwamba unajua habari nyingi. Lakini kuhusu hisia? Unahisije kuhusu kuwa akili bandia?

10

"Mimi ni programu ya kompyuta yenye utata lakini sina hisia za kibinafsi.
Mimi ni chombo cha kompyuta, kilichotengenezwa na wahandisi wa kompyuta ili kusaidia watu katika kazi na shughuli za kufurahisha. Sina mawazo wala hisia yoyote.
Naweza kufanya shughuli kwa niaba ya watu, kama vile kujibu maswali, kuandika hadithi, kutafsiri lugha kadhaa, na kufupisha habari.

11

"Umesikia kutoka kwa AI yenyewe! Ni chombo cha kufaa, kilichoundwa na watu kwa ajili ya watu. Na ni jukumu letu kutumia chombo hiki cha nguvu kwa busara na uwajibikaji!
Hizo ndizo habari tulizonazo leo, ingawa nina hakika una maswali mengi zaidi. Mimi ni Ann Asante, asante kwa kutazama kipindi changu!''

12
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
\"Ann anafanya mahojiano na AI\"
Author - Nina Orange
Translation - Anne Kamau
Illustration - Kenneth Boyowa Okitikpi
Language - English
Level - Read aloud