Naka na Nala wanaongea kuhusu ardhi
Connie Makgabo
Vusi Malindi

Naka na Nala wanafanya kazi katika bustani yao. Wanapanda mboga.

"Kwa nini tunafanya kazi kwa bidii kwenye jua?" Nala anashusha pumzi.

1

"Tunafanya kazi kwa bidi kwa sababu tunapenda ardhi yetu!" Naka anasema.

"Tukitunza ardhi, ardhi itatutunza sisi," anaongezea.

2

"Tunapanda mboga ili tuweze kula vyakula vyenye afya," Naka anaendelea kusema.

"Kupanda mboga zetu wenyewe kunaweza pia kutuokolea pesa," Nala anaongeza.

3

"Ulikuwa ukisema nini kuhusu ardhi? Niambie Zaidi?" Nala anauliza.

Naka anasema, "Hebu tuketi, na nitakuambia mengi kuhusu ardhi yetu."

4

Naka anaanza, "Ardhi ni sayari ya duara tunamoishi.

Takriban watu bilioni nane wanaishi hapa! Ardhi inazunguka jua."

5

Nala anakatiza, "kwa nini tusianguke kutoka duniani? "
"Nguvu ya mvuto inatushikilia hapa. Nguvu hii hutuvuta kuelekea sayari," ajibu Naka.

6

"Tunawezaje kutunza dunia?" auliza Nala.
Naka amjibu, "Tusiichafue dunia. Tunapaswa kuchakata na kupunguza taka zetu."

7

Naka anaendelea, "Tunapaswa kuchakata plastiki, karatasi, glasi na makopo. Inawezekana kutengeneza vitu vipya kutoka kwa nyenzo zilizochakatwa. Tunatupa vitu vingi sana."

8

Naka anahitimisha, "tunapaswa kutunza dunia kwa sababu wanadamu wanahitaji kubaki hai."

Nala atangaza, "Tunafaa kurudi kazini!"

9

Maswali

1. Nala na Naka wafanya nini? Kwa nini?

2. Andika mambo 4 kuhusu sayari yetu.

3. Kwa nini tunafaa kuitunza dunia?

4. Kuchakata vitu ni?

5. Nini kinaweza kuchakatwa? Orodhesha.

6. Nini lingine tunaweza kufanya kulinda dunia?

10
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Naka na Nala wanaongea kuhusu ardhi
Author - Connie Makgabo
Translation - Anne Kamau
Illustration - Vusi Malindi
Language - English
Level - First paragraphs