Naka na Nala Wazungumza kuhusu anga za nje
Refilwe Ramagoshi
Busisiwe Ndlovu

Nala na Naka wako katika kambi ya shule.
Wanaweka hema zao kisha wanatazama machweo ya jua.
'Inapendeza sana, Nala afurahi.

1

Wanatazama jua likizama chini ya upeo wa macho kuelekea magharibi.
"Kuna mwezi kamili usiku wa leo," anabainisha Naka wakati mwezi unapochomoza upande wa mashariki.

2

Watoto wanalala chini wakisoma anga ya usiku.
Naka anashangaa, "kuna nyota nyingi na zinangaa kama almasi!"

3

Anasema, "Mwezi unang'aa kwa sababu unaangaza mwanga wa jua.
Unapokuwa mwezi mzima, unaonekana kama mwezi mzima unawaka."

4

Nala akubaliana, "mwezi huzunguka dunia. Mara nyingine tunaweza kuona sehemu tu ya mwezi imeangaza, na inaonekana kama ndizi."

5

Anaendelea, "Mwezi unaonekana kama mpira wa miguu wakati wa mwezi kamili. Mwezi unapoisha, tunaona nusu ya mwezi. Ni kama umbo la ndizi."

6

Naka anasema akijivunia, 'Nilijua hilo! Pia nilijua kuwa mwezi huzunguka dunia na pamoja vyote huzunguka jua."

7

Nala anatabasamu, "Je, ulijua kwamba Jua ni nyota?"
Anaongezea, "Jua ni nyota kubwa ya gesi zinazowaka, zikizalisha mwanga na joto."

8

Naka anafikia, 'Bila mwangaza wa mji, tunaweza kuona anga ya usiku kwa uwazi. Anga ya nje huanza juu ya safu ya hewa karibu na dunia, lakini anga ya nje inaishia wapi?"

9

Nala anatabasamu, 'Tutakuwa wanaaga na tusafiri kwa ndege ya kasi zaidi. Tutapita sayari na nyota za mbali zaidi. Halafu tutajua anga za nje zinaishia wapi."

10

Maswali

1. Hadithi inawahusu nani? Wanafanya nini?

2. Mwezi kamili ni? Chora.

3. Mwezi huchomoza wapi?

4. Nyota iliyo karibu na dunia ni ipi?

5. Kuna sayari 8. Zitafute.

6. Chora picha ya jua na sayari.

11
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Naka na Nala Wazungumza kuhusu anga za nje
Author - Refilwe Ramagoshi
Translation - Anne Kamau
Illustration - Busisiwe Ndlovu
Language - English
Level - First paragraphs