Naka na Nala wanaongea kuhusu hewa
Ndivhuho Mutsila
Simon Mokoena

Naka na Nala wako katika uwanja mkavu, wakiwa wameketi chini ya mti.

Nala anaskia majani yakipepesuka kutokana na upepo mwanana.

1

"Sikiliza Naka, unaweza kusikia sauti ya majani?" Nala anauliza.

"Ndiyo, ninaweza kuyasikia na pia kuyaona yakisonga," Naka ajibu.

2

"Je, unakumbuka nini kinachofanya majani kusonga?" Naka anauliza.

"Ni wakati upepo unavuma na kupeperusha vitu," Nala anajibu.

"Ni hewa," Naka anasema.

3

"Hewa iko kila mahali, lakini hatuwezi kuiona," Nala anaanza.

Naka anakatiza, "Lakini tunaweza kuona na kusikia majani yakisonga!"

4

Nala anaendelea, "Hatuwezi kuona hewa, ila tunaweza kuona na kuskia athari za hewa ikisonga. Hiyo inaitwa upepo."

"Upepo ni hewa?" Naka auliza.

5

"Ndiyo," Nala anatabasamu.

"Hewa pia hushikilia matone madogo ya maji katika mawingu. Maji katika mawingu yanapozidi kuwa mazito, matone ya maji huanguka kama mvua."

6

"Hebu fikiria ikiwa sisi tunaweza kupaa angani katika puto la hewa moto. Puto hilo ni kama tone la maji na hewa inalishikilia juu," Nala anasema.

7

"Sis pia tunavuta hewa," Naka anakumbuka.

"Ndiyo, wanyama wote na mimea inahitaji hewa ili kuishi," Nala anasema.

"Tunahitaji hewa safi," Naka anakubaliana naye.

8

"Hatuwezi kuiona hewa, lakini imetengenezwa kutoka kwa kitu gani?" Naka anauliza.

"Hewa ni mchanganyiko wa gesi na chembe ndogo za vumbi," Nala anajibu.

9

"Dunia imegubikwa kwa hewa," Nala anasema.

"Hewa iko kila mahali. Hewa ya dunia inatanda kutoka hapa hadi angani," Nala anaongeza.

10

Hadithi inahusu nani? Wako wapi?
Nani ahitaji hewa? Nini hutengeneza hewa?
Hewa iko wapi? Mbona mvua huanguka?
Upepo ni nini? Tafuta hadithi kuhu upepo. Hewa safi ni nin?

11
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Naka na Nala wanaongea kuhusu hewa
Author - Ndivhuho Mutsila
Translation - Anne Kamau
Illustration - Simon Mokoena
Language - English
Level - First sentences