Jinsi ya kumsaidia mtu majini
Sea Rescue and Sean Verster

Ikiwa mtu yuko ndani ya maji, unaweza kutumia kijiti ili kumvuta kwenye usalama.

Usiingie kamwe majini ili kujaribu kuokoa mtu.

Ukiingia ndani ya maji, unaweza pia kuzama.

1

Ikiwa mtu anayehitaji msaada yuko mbali sana na wewe kuweza kufikia kijiti, unaweza kutupa kitu kinachoelea.

Tupa kitu ambacho anaweza kushikilia na kutumia kukaa juu ya maji. Unaweza kurusha mpira wa miguu au chombo tupu cha plastiki cha lita tano.

2

Ikiwa mtu anahitaji kuokolewa kutoka kwa maji, mwulize mlinzi au mtu mzima usaidizi. Kamwe usiingie majini kujaribu kuokoa mtu mwenyewe.

Unaweza pia kupiga nambari ya dharura ya kitaifa ya polisi.

3

Ikiwa mtu ameokolewa kutoka majini na hapumui, unapaswa kupiga simu kupata usaidizi.

Kisha unaweza kuanza Huduma ya Kwanza ya Mikono kwa kusukuma kwa nguvu na haraka katikati ya kifua chake. Usifanye mazoezi haya kwa mtu yeyote!

Unaweza kujua zaidi kutoka kwa Taasisi ya Kitaifa ya Uokoaji wa Bahari.

4
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Jinsi ya kumsaidia mtu majini
Author - Sea Rescue and Sean Verster
Translation - Ursula Nafula
Illustration -
Language - Kiswahili
Level - Read aloud