BINTI MREMBO
Fatma Maleta
Rob Owen

Habari, mimi ninaitwa Ndela Pittins kutoka kijijini huko nchini Afrika ya kusini.Sisi tunaishi maisha ya kawaida sana. Tumezaliwa wawili , mimi na mdogo wangu anayeitwa Eden. Lakini Eden ni mtundu sana duu!

1

Katika familia yetu tupo mimi, mama na mdogo wangu wa kiume , Eden .Miaka ya nyuma huko, baba yetu alifariki hivyo tumelelewa na mama yetu.Lakini bado imeendelea kuwa familia ya furaha.Mama yetu amehakikisha tunapata kila kitu na tunaishi maisha mazuri, ya furaha na amani .

2

Mama yetu alihakikisha tunapata kila kitu.Alifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunaishi maisha mazuri .Yeye nI shujaa, malkia wetu na rafiki yetu mkubwa sana .Kila tunapotaka ushauri , mama hutupa ushauri mzuri sana. Mama yetu hupika chakula kitamu sana hata huwa natamani zaidi.Mama ni mjasiliamali anayemiliki mgahawa uiitwao La Amore ambao ni mdogo lakini maarufu sana kijijini.Anatamani sana biashara yake iwe kubwa na maarufu zaidi Afrika kusini yote. Hiyo ndio ndoto yake maishani.

3

Nchini , Afrika kusini , nina marafiki wengi kutoka dini ,rangi na matabaka mbalimbali. Lakini wote tulicheza pamoja kwa furaha .Rafiki yangu Priya alikuwa mhindi, Robert mzungu, Lee mkorea na Tiana alikuwa amechanganyika na wengine walikuwa weusi kama mimi.Weusi uliongara , kama rangi yangu.
Dini , rangi wala makabila hayakututenganisha bali zilitufanya tupendane zaidi na kutuunganisha pamoja.

4

Upendo ni kitu muhimu katika maisha .Sisi kama watoto , tunapenda kufurahi na kuishi maisha yenye furaha siku zote. Watoto wengi walirukaruka na kufurahi pamoja tena kwa sauti mno.Kijiji chetu kilikuwa chenye furaha, kama nyumbani , tena chenye amani kuishi.Tulicheza sana mpira , kombolela, mdako na biringe bayoyo , biringe ba .Mara nyingine tuliogelea , kucheza ukuti ukuti na michezo mingi sana.

5

Kuna muda nilikuwa namkumbuka sana baba yangu .Mama huwa hapendi kumwongelea kwasababu bado anahisi maumivu sana.Nafikiri ana maumivu zaidi kuliko mimi na mdogo wangu Eden .Ila huwa anajitahidi kuwa jasiri.Wazazi wetu walipendana sana na furaha yao itadumu milele pamoja na sisi.

6

Mama yetu anasema kwamba uzuri wa mtu sio kwa muonekano wa nje bali kuwa na moyo mzuri na tabia nzuri.Pia anatuhamasisha mimi na mdogo wangu kusoma kwa bidii na kufanya kazi kwa bidii kwasababu hamna kitu cha bure maishani .Hivyo tunatakiwa kuwa makini , hasa kwa watu tusiowajua .Elimu ni muhimu kwa watoto wote duniani kwasababu itawainua na kuwajengea kesho bora zaidi.

7

Mama yangu amenihamasisha sana katika maisha .Tangu nikiwa mtoto nilikuwa na ndoto ya kuwa mlimbwende atakayewakilisha nchini yangu duniani.Hivyo nilipaswa kusoma kwa biddi shuleni.Pia nilishiriki mashindano mengi ya ulimbende .Mara nyingi nilifeli , nikakata tamaa.Lakini familia yangu walinihamasisha niendelee, nisikate tamaa. Mdogo wangu Eden siku zote alikuwa mstari wa mbele pamoja na mama wakinishangalia .Hii ilinipa moyo sana wa kuendelea hata nilipofeli.

8

Sikukata tamaa nikaendelea kujaribu mashindano mengi na mengi zaidi ya urembo na ulimbwende.Nikafeli mara nyingi tena , hat nikawa naona aibu na kulia sana.Lakini siku moja niliweza kufika kumi bora ya mashindano ya urembo hatimaye nikashika nafasi ya kwanza .Mama yangu alilia kwa furaha na mimi nikajikuta nalia tu.

9

Miaka miwili baadae , nikapata nafasi ya kushiriki mashindano ya urembo duniani ambapo nilishinda taji la Ulimbwende wa dunia kutoka Afrika kusini pale nchini Ufaransa.Nilifurahi sana siku hiyo yani mama na Eden walifurahi zaidi.Eden waacha aje jukwani nakumbatia , walimpiga vibaya mno mpaka nikasema
''Huyu ni mdogowangu, amefurahi , mpaka ameshikwa na ukichaa.'' ndio walimuachia.Basi watu wacha wacheke .Walicheka mpaka basi.Nilipotembea kijini wanakijiji walinipokea kwa furaha mno.

10

Ukifanya kazi kwa bidii , utavuna matunda yake .Nimeweza kujifunza vitu vingi sana , kimojawapo ni kwamba uzuri ni pale unaposaidia jamii yako , na watu wengine .Leo ninajivunia mwanamke niliyekuwa, nimepambana sana hadi kufika hapa .Sasa kila mtu anatakuwa binti mlimbwende lakini ulimbwende mzuri huanzia ndani yako . Kila mtu anaweza kuwa mzuri kwa kuwa na moyo mzuri , na matendo mazuri.Mama yetu anajivunia kuwa na watoto wachapakazi kama sisi

11

Mtu mzuri ni yule aliokuwa na moyo mzuri , mkarimu , mwenye upendo , ushirikiano na huruma kwa wengine .Huo ndio uzuri unaotakiwa , sio wa muonekano tu kama wengi wanavyodhani.

12

Nilianzisha shirika lisilo la kiserikali kwaajili ya kusaidia wakimbizi liitwalo UMOJA nikiwa na matumaini kuwa dunia itakuwa nzuri na salama zaidi kwaajili ya viumbe vyote tuishi kwa furaha , amani na upendo zaidi.

13

Mama yangu ameweza kukuza biashara yake sehemu kubwa ya Afrika kusini .Sasa anamiliki matawi kumi ya mighahawa na amepata mafaniko makubwa mno .Mdogo wangu Eden naye yuko chuoni , lakini humsaidia mama katika biashara zake kila anapopata muda.Mimi pia husaidia ninapoweza .Sasa tumehamia katika nyumba kubwa na nzuri mno .Leo nimekuwa nafuraha kwasababu ninahitimu shahada yangu ya elimu ya juu pale chuo cha Cape Town .Ni furaha ilioje kwa yule mtoto aliyekuwa na ndoto kubwa kuweza kuzifikia .Ninawahamasisha tusome na kufanya kazi kwa bidIi tufikie ndoto zetu.

14
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
BINTI MREMBO
Author - Fatma Maleta
Translation - Fatma Maleta
Illustration - Rob Owen, Vusi Malindi, Ruby Thompson, Catherine Groenewald, Jesse Breytenbach, Sayan Mukherjee
Language - Kiswahili
Level - Read aloud