"Njoo tucheze Kidalipo," kaka yangu aliniambia.
1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 12… …92, 93, 94, 95, 96, 100!
Kaka yangu alikuja kunitafuta. Nilikuwa nimejificha nyuma ya pazia.
Alinitafuta nyumba nzima.
Aliingia ndani ya chumba nilimokuwa nimejificha.
Nilitulia kabisa. Nilikuwa nikiwaza, "Atanipata."
Halafu, alitoka nje!
Nilikimbia nje. Nikapiga kelele, "Hukunipata!"