Tulikuwa tukiishi na Bibi yangu na mama yangu.
Binamu zangu, Kristina, Tandi na Junior na Shangazi waliishi nasi.
Bibi yangu angetufundisha michezo. Ulikuwa wakati mzuri sana.
Halafu Junior akaenda Malawi, naye Bibi pia akaenda Malawi.
Shangazi na Kristina pia wakaenda Malawi.
Halafu Tandi vilevile, akaenda Malawi.
Ilisikitisha kweli. Hakuna aliyeishi nasi.
Lakini, si mbaya sana, kwa sababu mama yangu bado yuko hapa nami.