

Ninapomaliza kuoga kwa maji moto, mwili wangu huwa majimaji na kuhisi baridi.
Ninajua anayesababisha mwili kuhisi baridi. Vayu, upepo!
Kwenye kikombe kuna maziwa moto sana. Baada ya muda, maziwa yanapoa.
Ninajua anayesababisha jambo hili kutendeka. Vayu, upepo!
Pazia za dirisha zinapapatika polepole zikinigusa uso.
Ni nani husababisha jambo hili kutendeka? Vayu, upepo!
Ninaona radi. Mawingu meusi yananikaribia.
Ninajua anayesababisha jambo hili kutendeka. Vayu, upepo!
Matawi yanayumbayumba na majani yanapepea. Maua yanadondoka kutoka mtini.
Ninajua anayesababisha haya yote. Vayu, upepo!
Tunapocheza nje, tunanukia pipi anazotayarisha mama.
Ninajua anayesababisha hili kutendeka. Vayu, upepo!
Bilauri iliyokuwa dirisahani, imeanguka na kuvunjika. Namshukuru Mungu haikuniangukia. Ninajua aliyesababisha ukatili huu. Bila shaka ni Vayu, upepo!
Firimbi imepulizwa. Gari la moshi linafika kituoni. Siwezi kuliona, lakini nausikia mngurumo wake.
Ninajua aliyesababisha haya. Vayu, upepo!
Haonekani. Hasikiki. Hufanya kazi zote kisirisiri. Anaweza kuwa ni nani?
Mimi ninamjua! Vayu, upepo!


