Mkoba uzungumzao
Caroline Lentupuru
Wiehan de Jager

Hapo zamani za kale aliishi jitu jike lililoitwa Motio.

Siku moja lilipokuwa likitembea kando mwa ziwa liliwaona wasichana watatu, Lisa, Vera na Elsa.

Likawauliza, "Ni nani kati yenu anayependwa na wazazi wote wawili?"

1

Lisa alijibu kwanza, akasema, "Mamangu hunipenda zaidi."

Vera naye akasema, "Babangu hunipenda zaidi."

Elsa akasema, "Baba na mama wananipenda sawa."

2

Motio alimwambia Elsa amfuate akamsaidie kuliinua tita la kuni.

Elsa alimfuata Motio bila kuogopa.

3

Walipotembea hatua chache, Elsa alimwuliza Motio, "Zi wapi kuni zako nikusaidie?"

Motio akajibu, "Ziko karibu na ile miti."

4

Walipofika hapo, Elsa akamwuliza Motio tena, "Zi wapi kuni zako?"

Motio akajibu, "Haziko mbali kutoka hapa."

5

Walipokuwa wakitembea, walikutana na mwanamume. Mwanamume huyo alimwuliza Motio, "Mtoto wako anaitwaje?"

Motio akajibu, "Anaitwa Mkoba Uzungumzao."

6

Elsa aliimba kwa sauti:

Mimi kamwe si mkoba.
Mkoba hauongei.
Ninaitwa Elsa.
Lo! Nyumbani, kuna
Mama nimpendaye,
Baba nimpendaye,
Kata nilinywealo maziwa.

7

Mwanamume huyo alipousikia wimbo wa Elsa, alimhurumia, akamwuliza amwelezee juu ya wazazi wake.

Alimnusuru kutoka kwa Motio na kumrudisha kwa babake na mamake. Wazazi wake walimshukuru mwanamume huyo na wakaishi kwa furaha na mtoto wao.

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Mkoba uzungumzao
Author - Caroline Lentupuru
Translation - Mutugi Kamundi
Illustration - Wiehan de Jager
Language - Kiswahili
Level - Longer paragraphs