

Hapo zamani, ndege aliyeitwa Mojo aliishi katika ufalme wa Baro. Kobe alikuwa rafikiye.
Mojo alikuwa mjumbe na alisafiri mbali kupeleka jumbe.
Siku moja, Mfalme Simba alimwita Mojo.
Mfalme Simba alimtaka apeleke ujumbe wa maana kwa Jamaa yake, Smba Marara, aliyekuwa mfalme kwenye ufalme tofauti.
Kobe aliposikia hivyo, alimwonea wivu.
Alimshauri Mojo, "Usiende. Ni mtego. Simba anakutuma wewe kama kafara."
Mojo aliogopa. Siku iliyofuata, alienda kwa jamaa yake Jimbi akamwambia alivyoambiwa na Kobe.
Jimbi hakumwamini Kobe.
"Nitakutayarishia mlo mtamu usiku wa leo," Kobe alimweleza Mojo alipokutana naye baadaye.
Mojo alienda nyumbani kwa Kobe kwa furaha kwa mlo.
Mojo alipokuwa akistarehe, Kobe alimtupia wavu akamnasa! Kisha alienda nje kutafuta kuni.
Mojo hakuweza kusonga. "Nisaidie, nisaidie!" alilia.
Jimbi alikuwa karibu na nyumba ya Kobe. Alimsikia Mojo akipiga kelele. Aliita, "Mojo? Mojo?"
"Jimbi! Njoo uniokoe!" Mojo alijibu.
Jimbi alienda kwa haraka mahali Mojo alikuwa.
Jimbi alimwokoa Mojo kutoka kwenye wavu.
Mojo alimshukuru Jimbi kisha akikimbia na kwenda zake.
Mojo alimwambia Mfalme Simba kuhusu jambo hilo. Mfalme alimfukuza Kobe kutoka kwenye ufalme wake.

