Zamani dunia ilikuwa mpya. Milima ilifunika ulimwengu kama blanketi.
Dunia ilikuwa na dimbwi kubwa. Lilikuwa na maji baridi yaliyotulia.
Nyoka wawili waliishi kwenye dimbwi. Mmoja mwenye nguvu, mwingine dhaifu.
Siku moja radi ilipiga. Nyoka wakaona ardhi na vitu tofauti.
Wakaamua kwenda kuishi kwenye ardhi.
Wakajikunjua wakaogelea. Wakaelekea kwenye mwangaza.
Mikia yao ikagawika wakawa na miguu. Wakapata pia mikono na vidole.
Wakageuka wakawa mume na mke. Wakatazamana, wakapendana.
Wakaamua kulinda wanyama na mimea. Wakafurahia jua.
Wakashikana mikono. Wakatembea pamoja kwenye ulimwengu wao mpya.