Zamani mamba aliishi karibu na mto na wanawe.
Aliwafunza wanawe kutowaamini binadamu. Binadamu walikuwa na bongo.
Siku moja, mwanamume mmoja alikuwa akivuka mto.
Mwanamume huyo alikutana na mamba katikati ya mto. Mamba alimshambulia.
Mamba alipokuwa karibu kumuua, alikumbuka maneno aliyosema babake. Alimwambia kila mara kuwa binadamu wana bongo.
Mwanamume huyo alimuahidi mamba kuwa angemletea bongo za binadamu. Mamba akamuacha huru.
Hadi leo, Mamba na wanawe bado wanasubiri kwenye ukingo wa mto kupokea bongo hizo.
Hadi leo, mamba wana hasira na binadamu. Hawakuwahi kupokea bongo walizoahidiwa.