

Siku moja, Mchungaji hakuwa na nyasi za kuwalisha nguruwe, kondoo na mbuzi wake. Pia hakuwa na nafaka za kumlisha kuku. Vilevile hakuwa na zizi la kuwaweka mifgugo.
Aliamua kuwauza ili wapate chakula na makazi bora.
Alisema, "Ninaweza kuwauza kila mmoja robo."
Lakini mnunuzi alitaka bei ya chini zaidi.
Mnunuzi akasema, "Ninataka mbuzi peke yake."
Mchungaji akajibu, "Wanyama hawa ni marafiki.
Ningependa waishi pamoja."
Basi Mchungaji akawauza kondoo, mbuzi na nguruwe kwa robo kila mmoja. Kisha akampatia mnunuzi kuku bila malipo. Alipokuwa akirudi nyumbani Mchungaji alikuwa na huzuni.
Aligundua kwamba wale hawakuwa wanyama tu. Walikuwa marafiki zake pia.
Alirudi akamrejeshea mnunuzi hela zake ili awachukue marafiki zake.
"Wanyama hawa sasa ni wangu," mnunuzi alisema. "Sitaweza kukurudishia."
Hata hivyo, mchungaji aliendelea kumsihi.
"Nimegundua kwamba wao si wanyama tu bali ni marafiki zangu," mchungaji alisema.
Mnunuzi aliuliza, "Mbona basi uliwauza?"
Jirani aliwasikia wakibishana akasema, "Nenda ujenge zizi, utafute nyasi na nafaka. Halafu, unaweza kuwarejesha wanyama wako."
Mchungaji aliwapenda sana wanyama wake. Alimrudishia mnunuzi hela zake.
Aliwatengenezea zizi zuri akawapa nyasi na nafaka.

