

"Mwaka huu tutakuwa na mkutano maalum wa familia," Mama Pembenyingi alitangaza. "Nani atakayehudhuria? Natumai Pembenyingi wote watakuwa. Ninawakosa binamu yangu," Kosi alisema. "Ninakosa zaidi upande wa familia yangu ya Pembenne," Mama alitabasamu. "Ndiyo, ni kitambo sana tangu tuwaone Mstatili, Mraba, na Msambamba," alisema Baba Pembenyingi. "Usisahau, wana watoto watatu sasa!" Mama alimkumbusha Baba.
"Na binamu wengine, je? Watakuja?" Fusi aliuliza. Mama alijibu, "Ndiyo, wao ni Pembenyingi, ingawa si Pembenne. Jina lao la ukoo ni Pembetatu. Watoto ni Pembetatu Pacha na Pembetatu Sawa." "Aa, ndiyo, familia ya Pembetatu!" alishangaa Fusi. "Lakini wanafanana sana na Pembenne." "La, sio kabisa," Mama alisema. "Pembetatu wana pande tatu, ilhali Pembenne wana pande nne, kama mimi."
Baba Pembenyingi aliongeza, "Nimefurahi kwa sababu binamu zangu wengine watatu watakuwa hapa: Pembetano, Pembesita na Pembenane. Wao pia ni wa familia yetu ya Pembenyingi." Vusi aliuliza, "Baba, mbona tunaitwa Pembenyingi?" "Kwa sababu tuna sura pande mbili. Tumeumbwa kwa mistari iliyonyooka, na maumbo yetu yamefungika, kama unavyoona, mistari yetu yote imeunganika. Binamu yetu Pembetatu, Pembenne, Pembesita, na Pembetano wote watatutembelea," Baba alijibu.
"Je, ulisema kuwa Pembenane atakuja? Yeye pia ni jamaa yetu?" Khosi aliuliza. "Bila shaka, binti yangu, ukimtazama, utajua kwamba ni wa familia yetu. Unastahili kuangalia kwa makini idadi ya pande ambazo binamu yako wanazo, au hutaweza kuona tofauti. Binamu Pembenane ana pande nane kwa sababu jina lake linamalizika na nane," Baba alisema.
"Sawa, na Pembetano na Pembesita, je?" Vusi aliuliza. "Binamu Pembesita ana pande sita kwa sababu jina lake linamalizika na sita," Baba alijibu. "Pembetano wana pande tano. Mwalimu wetu alituambia kwamba tano inatokana na pande hizo
tano," aliongeza Khosi. "Kumbuka kwamba tatu na nne ndizo zinafanya binamu yako Pembetatu na Pembenne kuwa tofauti.
"Baba, Pembesaba ana pande ngapi?" Vusi aliuliza. Baba alicheka akasema, "Sitakwambia. Kumbuka tulipiga picha zake tulipokuwa kwa harusi ya mjombako. Ningependa uitazame picha ile kwa makini kisha unieleze unachoona. Vusi aliitazama picha haraka halafu akajibu, Pembesaba ana pande saba!" Khosi aliongeza, "Ndiyo, kumbuka mwalimu wetu alituambia kuwa saba inatokana na idadi sab."
"Aa mke wangu, unaona jinsi watoto wetu walivyo werevu? Je, kumi ina maana gani?" Baba aliuliza. "Pembe kumi!" Vusi na Khosi walisema. "Ndiyo, hiyo ndiyo sababu binamu yenu anaitwa Pembekumi. Lakini, hatakuja kwa sababu ataiwakilisha timu ya waogeleaji. Kuna Pembekumi wachache sana shuleni kwao," Mama aliwaambia.
Watoto walisema, "Mama na Baba, tunaweza kumualika rafiki yetu Mduara?" Wazazi wao walikubali Mduara kujiunga nao kwa sherehe. Wakati huo, waliusikia mlango ukibishwa. Baba alienda kujua ni nani. "Pembenne wako hapa! Karibu! Karibu!" Baba alishangilia.
Familia yote inaruka kuwasalimu Mraba, Mstatili, na watoto watatu wa Msambamba. Pembenne wanafurahi kuwa wa kwanza kufika.
Familia ya Pembetatu inabisha mlango muda mfupi baada ya kufika kwa Pembenne. Pembetatu pacha na Pembetatu sawa wamechoka baada ya safari ndefu. Lakini, wamefurahi kuwa pamoja na familia nzima.
Hatimaye, Pembenane na Pembesaba wanawasili pamoja na wanao, Pembetano na Pembesita. Pia wemewaleta Miraba watatu. Pembenane anaeleza, "Natumai si tatizo kwamba wana Pembenne watatu kutoka kijijini wamekuja nasi. Hawajawahi kwenda jijini." Mama alitabasamu, "Marafiki na familia wanakaribishwa hapa kila wakati." Aliwatuma watoto wote nje kucheza.
"Tutacheza mchezo gani?" Vusi aliwauliza watoto wengine. Pembetatu sawa alisema kwa furaha, "Hebu tucheze mchezo wa maumbo!" Watoto wote wa Pembenyingi walianza kucheza mchezo huo. "Ninaweza kucheza nanyi? Mimi pia ningependa kucheza mchezo wa maumbo," Mduara alisema. Vusi alimjibu, "Aibu kubwa, samahani, huwezi kucheza mchezo huo rafiki yangu." Mraba mmoja aliongeza, "Huoni umbo lako, wewe si wa familia ya Pembenyingi. Duara hawawezi kucheza mchezo wa maumbo."
Mduara alihuzunika sana kwa kuachwa nje ya mchezo. Lakini, mchezo haufurahishi sana mmoja akiachwa nje. Vusi alisema, "Ni heri tucheze mchezo ambao Mduara pia anaweza kucheza." Kwa hivyo, Pembenyingi na Mduara walicheza pamoja kwa furaha hadi chakula kitamu kilipokuwa tayari.
Tafsiri yako hapa
Tafsiri yako hapa
Tafsiri yako hapa

