Bi Kizee alikuwa na mjukuu aliyeitwa Noah. Alimpatia Noah yai.
Noah alikutana na wachuma matunda damu. Walilivunja yai hilo.
Noah alilia, "Yai lilikuwa la kulipia mahari!"
Wachuma matunda damu walimpatia Noah fimbo.
Noah aliwakuta wajenzi. Wakaivunja fimbo ile.
Noah akalia, "Fimbo hiyo ilikuwa ya wachuma matunda damu!"
Wajenzi walimpatia Noah kifurushi cha nyasi.
Noah akamkuta mchungaji wa ng'ombe. Ng'ombe akaila nyasi hiyo.
Noah alilia tena, "Ile nyasi ilikuwa ya wajenzi!"
Mchungaji alimpatia Noah ng'ombe.
Noah alipata sherehe ya harusi. Walimchinja yule ng'ombe.
Noah alilia, "Yule ng'ombe alikuwa wa mchungaji!"
Familia ilimpatia Noah bi harusi.