Mod alikuwa amechoka kuishi majini.
"Jihadhari. Ngozi yako itanyauka," Kasa alimwonya.
Lakini, Mod alitaka kujua. Aliruka akaenda zake.
Alitazama kila mahali.
Alikuta kinyonga wa kizambarau. Alikuwa kando ya dimbwi la maji.
Kinyonga aligeuka rangi ya waridi! Mod aliruka mbali naye.
Alimwona fisi akikoka moto.
Moto ulienea karibu na Mod. Aliogopa.
Moto uliichoma ngozi yake. Aliruka ndani ya dimbwi la maji.
Lakini ngozi yake ilikuwa tayari na malengelenge.
Mod alipata ngozi kavu na mbaya. Alianza kuishi miambani.
Vyura wachache wana ngozi nyororo. Wanaishi majini.