

Hapo zamani za kale, Ndovu na Sungura walikuwa marafiki wakubwa sana. Walikuwa na ngamia, ng'ombe na kondoo wengi.
Walilisha wanyama hao katika bonde la Kingilo. Wakati mwingine waliwapeleka wanyama milimani kulikokuwa na nyasi na maji kwa wingi.
Wanyama walipokula, Sungura na Ndovu walicheza. Walipenda sana kucheza mpira wa miguu.
Kila walipocheza, Ndovu aliingiza mabao mengi kumliko Sungura. Sungura alikasirishwa mno na hali hiyo.
Siku moja Sungura alimwuliza Ndovu, "Ni nini kinakuwezesha kuwa mwingizaji goli maarufu?" Ndovu alimjibu, "Ni miguu yangu minono."
Siku iliyofuata, Sungura alipendekeza washindane mbio. Ndovu alikubali na wakaanza mbio.
Sungura alishinda mbio zote. Ndovu alikasirika. Hakuwahi kushindwa. Alimwuliza Sungura, "Ni nini kinakuwezesha kuwa mkimbiaji maarufu?"Â Sungura alijibu, "Ni miguu yangu myembamba."
Ndovu alimwuliza, "Nitawezaje kupata miguu myembamba?" Sungura alimjibu, "Ni rahisi, nitakuonyesha. Tafuta kuni ukoke moto."
Ndovu alikusanya kuni akakoka moto mkubwa. Sungura alimwambia, "Sasa iweke miguu yako ndani ya moto." Ndovu alisimama ndani ya moto. Alipiga kelele, "Naungua! Naungua!"
Sungura alifurahi. Alimhimiza Ndovu aendelea hivyo hivyo maanake hivyo tu ndivyo miguu yake ingelikuwa myembamba.
Miguu ya Ndovu ilijeruhiwa vibaya akaondoka motoni. Hakuweza kusimama kwa hivyo alilala chini.
Ndovu aliketi kwa siku nyingi kabla kuweza kusimama.
Hatimaye, aliweza kuchechemea na kwenda nyumbani kwa familia yake.
Sungura alimwomba Ndovu msamaha. Hata hivyo, Â Ndovu na Sungura si marafiki tena.

