Mama abadilika
Ursula Nafula
Catherine Groenewald

Mama alipokuwa msichana, nilienda naye kuwatembelea marafiki zake.

1

Tulienda pamoja sokoni kununua mboga.

2

Alimpeleka ndugu yangu mdogo mjini.

3

Alinifunza majina ya mimea.

4

Mama alipoanza kuzeeka, mgongo wake ulipinda.

5

Aliketi nyumbani na kuzungumza na watoto wa majirani.

6

Alikuwa mgonjwa mara kwa mara.

7

Wajukuu wake walimtembelea wakati wa likizo.

8

Alitembea kwa shida.

9

Majirani walimnunulia maziwa dukani.

10

Mama alipokuwa msichana, alikuwa mwenye nguvu.

11

Sasa amekuwa mkongwe, amekuwa mnyonge.

12
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Mama abadilika
Author - Ursula Nafula
Translation - Ursula Nafula
Illustration - Catherine Groenewald, Jesse Breytenbach, Rob Owen, Wiehan de Jager
Language - Kiswahili
Level - First sentences