Aina ya meno
Zanele Buthelezi
Rob Owen

Meno ya mamba ni makali.

Mamba huishi wapi?

1

Meno ya simba vilevile ni makali.

Simba hula nini?

2

Papa ana meno makali zaidi.

Papa huishi wapi?

3

Meno ya ng'ombe husaga chakula.

Ng'ombe hula chakula gani?

4

Ndege hana meno.

Je, ndege hula namna gani?

5

Meno ya panya ya mbele ni makubwa.

Panya hula chakula gani?

6

Watu huwa na meno 32.

Nilipokuwa mdogo, nilikuwa na meno ya mbele.

7

Baadaye, meno yangu ya mbele yaling'oka.

Je, wewe una meno yako yote?

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Aina ya meno
Author - Zanele Buthelezi, Thembani Dladla, Clare Verbeek
Translation - African Storybook
Illustration - Rob Owen
Language - Kiswahili
Level - First words