

Hapo zamani za kale, Palitokea familia moja yenye upendo. Katika familia hiyo, Waliishi shangazi Lusia, Mjomba Lusia na Lusia.
Lusia ni mtoto yatima, mama yake na baba yake walifariki kwa ajali.
Lusia yuko darasa la tatu katika shule ya msingi Elimu bora na anamiaka nane.
Shangazi na mjomba Lusia, hawakuweza kupata mtoto. Lakini, Walimchukulia Lusia kama mtoto wao.
Walimpeleka shule, Walimpa chakula na kila alichohitaji walimpatia.
Siku moja,Shangazi Lusia alijisikia vibaya na kuanza kutapika.
Lusia alikuwa shuleni.
Mjomba Lusia alikuwa kazini.
Shangazi Lusia aliamua kumpigia mjomba Lusia.
Mjomba Lusia alipopata tarifa hizo, aliamua kurudi nyumbani na kumpeleka shangazi Lusia hosipitalini.
Baada ya vipimo, Ilionekana kuwa shangazi Lusia ni mjamzito.
Daktari aliwapongeza na kuwapatia maelekezo ili mtoto akae vizuri mpaka kujifungua.
Baada ya Lusia kurudi kutoka shuleni, hakuwakuta walezi wake nyumbani. Aliamua kuwasubiri.
Baada ya muda mfupi, mjomba na shangazi yake walirejea nyumbani.lakini hawakumweleza chochote.
Baada ya miezi 9,Siku ya tarehe 3 mwezi wa 3 mwaka 2002, Walijaliwa kupata watoto wawili, Wakike na wakiume.
Mtoto wa kiume Walimpatia jina la Nake na wakike aliitwa Upendo.
Baada ya siku kadhaa, mambo yalianza kubadilika. Shangazi na mjomba yake hawaku mjali tena bali walimtesa.
Siku moja mjomba Lusia alienda shuleni na kuomba uamisho. Uamisho huo ulikuwa wakuamia shule nyingine lakini walimuachisha shule kabisa.
Kisha alienda nyumbani na kumwambia Lusia kuwa, hataenda shule tena. Aliendelea kunyanyasika na kuteswa.
Alifanya kazi kubwa na kupatiwa chakula kidogo.
Siku moja mama mkubwa yake alimtembelea, akamkuta Lusia akiosha vyombo wakati mjomba na shangazi yake hawapo.
Lusia alifurahi kumuona mama mkubwa yake alimkimbilia kwa furaha, " kwanini hujaenda shule? " mama mkubwa wake alimuuliza. Lusia alimweleza kilakitu kilicho tokea.
Mama mkubwa wake aliamua kumpigia polisi na kuwaeleza kila kitu kwa haraka.
Mama mkubwa yake aliwaambia polisi wajifiche.
Baada ya muda kidogo, shangazi na mjomba Lusia walirejea.
Polisi waliwakamata haraka na kuwapeleka kituo cha polisi.
Kwanzia siku hiyo, Lusia alienda kuishi na mama mkubwa wake waliishi kwa furaha,mama mkubwa wake ana mtoto mmoja aitwae Mwane.Mwane alikuwa darasa la 5.
Mama mkubwa Lusia aliamua kuishi na watoto wa shangazi na mjomba Lusia.
MY NAME IS ESTHER HENDRY. I HAVE TEN YEARS OLD. MY SCHOOL NAME IS MEYER'S PRIMARY SCHOOL. I LIVE IN MONDULI ARUSHA.

