

Mimi Esther Hendry ninaona changamoto katika jamii yangu.
Watoto wadogo wanajihusisha na kuvuta bangi,kunywa pombe, kubaka na kulawiti watoto wakiume.
Tunatakiwa kusaidiana na jamii ilituweze kutatua changamoto hii kwasababu wengi wanapoteza ndoto zao za msingi.
Ili kutatua changamoto hii tunatakiwa kusaidiana na serekali ili mtuhumiwa akifanya kosa apelekwe kituo Cha polisi.
Bila kufanya hivyo watu watapata magonjwa,watapoteza ndoto zao za msingi na wengine kufariki.
Kufariki inatokana kwasababu mtu anaweza kukubaka au kukulawiti iliupate maradhi aliyokuwa nayo yeye ilikupoteza ndoto yako.
Ilikuepuka vitendo hivyo tunatakiwa kuwasikiliza wazazi,tusitembe usiku na tusitembe vichochoroni.
Tunatakiwa pia tukiona mwenzetu ananyanyasika tunatakiwa tumsaidie na mtuhumiwa apelekwe kituo cha polisi.
Hii pia itasaidia mtoto ajiamini na ataendelea na ndoto zake.
Mtoto anahaki ya kupatiwa elimu.
Serekali inatakiwa kutulinda ili tukae kwa amani.
Wazazi pia wanatakiwa kuwapatia watoto elimu na sio kuwaozesha.
MY NAME IS ESTHER HENDRY, l AM lN CLASS FIVE PUPIL.I HAVE TEN YEARS OLD. I AM THE FIRST CHILD IN MY FAMILY

