TUMEPIGA HATUA KATIKA SWALA LA MTAZAMO WA KIJINSIA
Sayuni Ronald
Sayuni Ronald

Mimi kama Sayuni nimejifunza vitu vingi katika mada ya mitazamo ya usawa wa kijinsia katika jamii yetu nimeelewa kwamba tusiwabague tupende jinsia zote.

1

Katika Jamii tusiwe wabaguzi wala tusiwe wagomvi tupendane.

2

Ubaguzi upingwe na tusiwabague walemavu watu wote wasomeshwe bila wanafunzi kuwakatisha tamaa.

3

Kwa kuwaambia maneno mabaya kwa mfano wewe huna akili,kichwa maji ,kichwa boga.

4

Watu wenye ugonjwa wa ngozi wananyanyaswa kwa kupewa kazi wasizoweza kuzifanya.

5

Ubaguzi unaweza kutokea kwa mfano wakike apelekwe shule.

6

Mtoto wakiume anambiwe aende kuchunga mfugo au anambiwa aende kufanya kazi ili familia ipate chakula.Pia,anaweza kumwambia alinde nyumba.

7

Anaweza kuambiwa afanye kazi kwa ajili ya ada ya mdogo wake na viatu vya mdogo wake.

8

Mama anampa vitu vya kuuza kwa mfano vitunguu,barafu na mboga na akirudi nila hela anampiga.

9

Akirudi bila hela anapigwa na humwamwambia kesho ukirudi bila hela usije nyumbani kwangu.

10

Mimi ninaitwa Sayuni .Ninasoma shule ya msingi Ngarash .Ninatokea Monduli. Ninamiaka 12.

11
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
TUMEPIGA HATUA KATIKA SWALA LA MTAZAMO WA KIJINSIA
Author - Sayuni Ronald
Illustration - Sayuni Ronald
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs