

Kwa mimi ninavyoona watoto wa kike wanateseka kwa kubakwa na kufanyiwa matendo maovu ambayo hawajatamani kufanyiwa.
chanzo cha watoto wa kike kubakwa, ni watoto wa kike kupita kwenye kundi la wahuni na wavuta bangi akiwa amevaa nguo fupi.Hivyo unakuta kile kitendo kinawatamanisha wale wahuni na mpaka kupelekea kukukamata na kukubaka.
Na swala la ukeketaji kwa mimi ninavyoona ni ukosefu wa elimu katika jamii.
Kwa sababu jamii ingekuwa na elimu wasingefikiria kufanya hivyo.Ukeketaji unamadhara mengi kama vile kupoteza damu nyingi na kupoteza maisha.
Pia kwa watoto wa kiume wanafanyishwa kazi ngumu kuzidi umri wao.
wengine wanaambiwa wasiende shule wakatafute ela ya chakula cha nyumbani.
pia wanawake nawanaume wanavuta bangi na kunywa pombe.
Swala la ubakaji tunashauriwa wanajamii kuwa na umakini wa juu kuhusu watoto wa kike avae nguo zinazomsitiri mwili mzima.
Swala la ukeketaji tunawashauri wazazi wapate elimu na hasara za ukeketaji.
Pia watoto wa kiume kuacha shule inatokana na umasikini hivyo tunawashauri serikali kutoa michango kwa familia zisizo jiweza.
Tunawashauri serikali wawe makini na hao watu ikiwezekana wapelekwe polisi wakakanywe.
KWA MAJINA NINAITWA KELVIN YONA.NINASOMA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI NGARASH.MIMI NI MTOTO WA PILI KWENYE FAMILIA YANGU.NINA MIAKA 13 KUMI NA TATU.

