Binti na nyoka.
Esther Hendry
Esther Hendry

Paukwa,Pakawa.
Hapo kale, palitokea familia Moja. Katika familia hiyo walishi bibi na babu Sakina na Sakina.

1

Wazazi wa Sakina walimfukuza Sakina baada ya kugundua Sakina ni mlemavu wa ngozi.

2

Kwa hiyo, bibi na babu yake Sakina waliamua kumchukua kumlea. Walimpenda sana.

3

Watu pia kwenye jamii yao walimcha, walimtukana na wengine walimwagia uchafu.

4

Sakina alikuwa na kipaji Cha kuimba, bibi na babu yake walipenda nyimbo zake na kila alipokosea walimrekebisha.

5

Katika Kijiji hicho, palikuwa na mto mkubwa.Katika mto palikuwa na nyoka mkubwa.

6

Nyoka huyo, alikuwa aking'ata watu ambao wanaenda kuchota maji hapo.

7

Watu wa kijiji hiko waliamua kuhitisha mkutano kuhusu nyoka huyo.

8

Sakina alinyoosha mkono na kusema "Mimi nitamuuwa nyoka kwa kutumia filimbi."

9

Watu walimcheka kwa kejeli.Bibi na babu yake walimzuia kwa kuogopa ukali wa nyoka huyo.

10

Kiongozi wa mkutano alimwambia "Je,unaweza kweli kumuuwa nyoka huyo?" Sakina alijibu,"Ndiyo nitaweza kumuuwa."

11

Kesho yake, Sakina alichukuwa mshale pamoja na filimbi. Bibi na babu yake walimwambia awe makini.

12

Alipofika pale , alipiga filimbi. Nyoka alimfuata Sakina ,akachukuwa mshale na kumlenga kichwani na akafanikiwa kumuuwa nyoka.

13

Sakina alirudi kijijini akiwa ameshikilia kichwa cha nyoka.Kwanzia siku hiyo watu walimuheshimu.

14

MY NAME IS ESTHER HENDRY. I HAVE TEN YEARS OLD. I AM IN CLASS FIVE IN MEYER'S PRIMARY SCHOOL. AND I LIVE IN MONDULI VILLAGE.

15
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Binti na nyoka.
Author - Esther Hendry
Illustration - Esther Hendry, Joseph Jonathan
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs