Tumepiga hatua kubwa katika swala la kijinsia kwa sababu tumejifunza vitu vingi kuhusu jinsia.
Na pia, tumejifunza namna ya kusaidia wenye changamoto kuhusu jinsia zao.
Tunasaidiana kwa kutoa taarifa kituo cha polisi.
Au kuomba msaada kwa jamii.
Na pia, tunaweza kumsaidia mtoto mwenzetu.
Tunaweza kumsaidia mwenzetu kwa kuomba msaada kwa jamii ili aweze kuishi kwa furaha na atimize ndoto zake.
Tunaweza pia kushirikiana na jamii kuhusu maswala ya kijinsia.
Na pia tunaweza kuelimisha jamii kwa kuwaonya watoto wa jinsia zote wasifanye na wasitende matendo yasiyo ya kimaadili.
Tunaomba msaada kwa serikali ili mtuhumiwa akimtesa mtoto yeyote apelekwe kituo cha polisi.
Sisi kama watoto, tuna ndoto nyingi ambazo tunatamani kuzitimiza.
Tunatakiwa pia kusoma kwa bidii ili kufikia ndoto zetu za msingi.
My name is Esther Hendry.I have 10 years old.I leave in Monduli village.My School name is Meyer's.