

Hapo kale palikuwapo na kijiji cha Mwendapole .Katika Kijiji hicho palikuwa na familia ya mzee Swaga ilikuwa familia yenye ushirikiano.
Katika familia hiyo palikuwa na mjukuu aitwaye Amani.
Amani alikuwa mtoto aliyekuwa yatima, mama na baba walifariki kwa moto.
Alipokuwa akiishi kwa babu alikuwa babu alikuwa mzee sana .Kwa kuwa ameishi miaka mingi .
Baada ya miezi 8 babu yake Amani alipoteza maisha kwa ugonjwa wa KANSA.
Amani alipelekwa kituo cha kulelea wa watoto yatima na kuishi huko.
Lakini palikuwa na ndugu za mamaye baada ya miaka 15 walijitokeza baba na mama yake mkubwa walijitokeza .Baba na mama yake mkubwa walikuwa matajiri sana.
Walikuwa na majumba makubwaWalikuwa na watoto wawili majina yao niJuliana naJaneth .Walikuwana umri wa miaka 15.
Katika nyumba ya mama na baba yake mkubwa Amani palikuwa na wafanyakazi wawili .
Walipofika nyumbani Amani alikaa kwa siku mbili .Wakamwambia wewe hustahilikuishi katika nyumba hii.Wakampakampati kazi nyingi kama vili kufyeka nyasi,kupika, kuosha vyombo kudeki . Hawakumpatia chakula kwa wakati mpaka ika pelekea ugonjwa
Alianza kunyong'onyea kiafya mpaka akaenda kuomba msaada kwa jirani aliyekuwa masikini.Alikuwa hana nyuma wala mbele alikuwa akiokota kuni kwenda kuwapikia watoto wake .Baada ya kumuona alimsaidia na kumpeleka hospital na Amani kupata afya
Mimi ninaitwa Sayuni Ronald Matowo .Ninasoma darasa la tano ni mtoto wa mwisho katika familia yetu nina miaka 12.

