Maisha Yangu ya Shule ya Bancroft
Makusaro Shank Lauwo
Meku Shank Lauwo

Kila siku, napanda basi kwenda Bancroft. Halafu nikifika shuleni Bancroft nakaa kwenye gym nikisubiri walimu. Halafu tunakaa wakati tunasubiri walimu.

Madarasa ya chekechea yako 4. Kuna darasa la Ms. Bethea, kuna darasa la Ms. Shanna, kuna darasa la Ms. Josie, na mwisho ni darasa la Ms. Ria.

1

Halafu mwalimu anatuambia tusimame halafu tunaenda darasani. Halafu tunaenda kuvua nguo zetu za nje, tunapeleka ajenda na chupa zetu kwenye vikapu. Halafu tunachukua lunch box zetu. Halafu tunakula snack.

2

Halafu wawili ambao wamemaliza snack wanapeleka folder ofisini. Halafu wale watoto wawili waliopeleka folder wanarudi na kusoma vitabu kama wenzio wengine.

Halafu baada ya hapo tunaenda kusikiliza muziki na kusoma kitabu.

3

Halafu kama kuna gym, tunaenda kwenye gym. Halafu kama hamna gym, hatuendi kwenye gym, tunacheza ndani.

Halafu baada ya kucheza ndani, tunaenda kujiandaa kucheza nje. Tunavaa kwa mfano koti, buti, snowpants, scarf, kofia, gloves.

4

Halafu tunaenda kupanga mstari tukiwa tunasubiri wenzetu. Halafu Ms. Zayne anatupeleka nje.

Halafu tunaenda kucheza nje. Siku zingine kukiwa na barafu tunaenda nje. Siku zingine kukiwa kuna barafu hatuendi nje.

5

Halafu wakati wa kurudi darasani kutoka kucheza nje, tunapanga mistari.

Baada ya kupanga mstari, kama tuna darasa la muziki baada ya kucheza nje tunakuwa wa kwanza kuingia ndani. Kama hatuna muziki baada ya kucheza nje, tunaenda darasani, halafu tunacheza.

6

Halafu kama tuna darasa la muziki, tunaenda darasa la muziki. Tukishamaliza darasa la muziki, tunaenda kula lunch.

Kama hatuna darasa la muziki, tunacheza ndani. Ms. Shanna anatoa vitu vya kuchezea. Halafu tunaenda kula lunch.

7

Halafu baada ya lunch, tunaweza kula snack au hapana. Mwalimu anatuambia twende kupanga mstari saa ngapi, kama anasema hapana hatuendi, kama anasema eee tunaenda.

Watoto wote wakishaisha, mwalimu mmoja kati ya wale wanne anasafisha meza zote.

8

Mwalimu akishatuambia tusimame, tunaenda kuweka lunch boxes kwenye shelfu, halafu tunapanga mstari tena na kwenda nje.

Halafu tukishafika nje, tunacheza. Nacheza na Aristide, pia nacheza na Ayah.
Halafu muda wa kwenda ndani ukifika tunaenda ndani.

9

Halafu tukishafika ndani, tunasikiliza muziki na kusoma vitabu. Halafu tunaenda nje tena halafu nacheza tena na Aristide.

Halafu tukishafika ndani tena, tunacheza. Ms. Shanna anatoa vitu vya kuchezea. Halafu baada ya kucheza, tunafanya clean up.

10

Jules anaita agendas na kuzigawa na Lucas anawapa wote chupa za maji.

Halafu tunaanza kuvaa nguo za nje, kwa mfano koti, buti, snowpants, scarf, kofia, gloves. Busers na walkers wanavaa hizi nguo zote.

11

Daycare wanaweza wakavaa snowpants au wasivae kwenda daycare. Daycare wanavaa begi na koti nyuma ya begi kwenye vichwa.

Na wote, kabla hawajaenda, walkers, busers, na daycare, wanaweka viatu juu ya bench.

12

Busers wanapanga mstari kwenye gym, walkers wanakaa kwenye lunch tables za wakubwa siyo lunch tables za chekechea. Halafu daycare wanasubiri kwenye benches.

Busers wanaitwa mmoja mmoja. Wanaitwa 208, 201, 214, 215, 230, 211.

Nampenda Ms. Shanna.

13

Makusaro (Meku) Shank Lauwo ni mwandishi na mchoraji mwenye miaka 5. Anasoma darasa la awali katika Shule ya Bancroft mjini Montreal.

Hiki ni kitabu chake cha nne. Vya mwanzo ni 'The Artist Who Painted a Blue Horse,' 'Safari ya Kuja Montreal,' na 'Kitabu cha Hisabati.'

14
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Maisha Yangu ya Shule ya Bancroft
Author - Makusaro Shank Lauwo
Illustration - Meku Shank Lauwo
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs