Lugha za Maisha Yetu
Wasichana wa Shule ya Msingi ya Mwasi Kaskazini
Klabu Ya Hadithi Zetu

Ninaitwa Loveness. Ninajua lugha mbalimbali kama Kichaga, Kimbulu, Kimaasai, Kiswahili, Kifaransa, na Kihindi. Ninatumia Kiswahili nikiwa na marafiki, walimu, na wazazi na hata kusalimia watu wakiwa njiani. Ninatumia Kichaga nikiwa na bibi yangu. Ninamsalimia Kwamza maye na yeye anaitikia Naiyo maye.

Ninatumia Kiingereza nikiwa na mwalimu darasani. Good morning. How are you? I am fine.
Ninatumia Kimbulu nikiongea na mama yangu kwa sababu mama ni Mbulu. Niliomba

1

anifundishe na ananifundisha. Salamu ni Laway. Kuitikia ni Sayuu. Na Idorii na Idomaa. Ahsante ni Naas.
Ninatumia Kifaransa nikiwa na mwalimu tunavyojadiliana kuhusu lugha. Salamu ni Comment ca va. Anaitikia Ca va bien. Lugha nyingine ni Kihindi: Namaste. Kimaasai ni Takwenya na mwingine anaitikia Iko.

Nyumbani ninatumia Kiswahili kingi na Kichaga kidogo. Karatu ninatumia Kiswahili na Kimbulu. Monduli ninatumia Kiswahili kidogo na Kimaasai kingi.

2

Kiswahili kinathaminiwa shuleni kwa sababu ni lugha ya taifa letu la Tanzania. Pia Kiingereza kinathaminiwa japokuwa ni lugha ya kikoloni lakini bado tunaendelea kujifunza.

Mbeleni ninataka kujua language nyingi na kujua kuziandika kama Kiarabu, Kichina, Kifaransa, Kihindi, n.k. kwa sababu ndoto yangu ni kuwa daktari. Sitatibu watu wa taifa langu tu, nataka kuwa daktari wa mataifa mengi. Na nikikutana na watu wenye lugha za makabila nitawaelewa.

3

Nitafanya bidii kusoma vitabu vya nchi mbalimbali na kuomba watu wenye uzoefu wanifundishe. Nikiwa katika kila nchi nitajifunza lugha za nchi hiyo.
Napenda kuongea lugha zangu. Sitaweza kuziacha zipotee au nizisahau. Nitawafundisha watoto, wajukuu, vitukuu, na watoto wa vitukuu.

Tunaweza kutunga na kuandika vitabu kuhusu jinsi ya kuthamini lugha. Mfano wa kuthamini na kuendeleza lugha ni kufundisha watoto wetu na watoto wetu wawafundishe watoto wao.
Naas. Thank you. Asante.

4

Ninaitwa Treasure. Ninajua lugha za Kiswahili, Kichaga, Kimaasai, Kiingereza, Kimbulu, na Kiha. Nimejifunza Kiswahili kupitia nyumbani. Nimejifunza Kiingereza shuleni, kwa mfano Good morning.

Nimejifunza Kichaga kutoka kwa bibi, mama, na majirani. Kwa mfano Kwamza mae – Naiyo mae. Nimejifunza Kimaasai nikiwa shuleni na maktabani. Pia nimesikia wanafunzi wenzangu, kwa mfano Takwenya – Iko. Nimejifunza Kimbulu kutoka kwa Loveness

5

shuleni, kwa mfano Aidorii – Aidomaa.
Ninajifunza Kiha. Siku sio nyingi ninaamini nitajua lugha yangu. Ninafanya uchunguzi kwa wazazi kusudi kujua lugha zangu na nyingine.

Lugha yangu ya Kiha ina umuhimu kwenye maisha yangu kwa sababu ya kuongea na jamii yangu na wazazi wangu. Ninaithamini lugha yangu kwa sababu ya kuelimisha familia yangu na jamii nyingine.

Wazazi huthamini lugha za Kichaga, Kiha, na Kiswahili.

6

Mlezi wangu, ambaye ni bibi, huithamini lugha ya Kichaga. Kwenye ofisi za serikali huthamini lugha za Kiingereza na Kiswahili kwa sababu wakoloni waliendeleza lugha ya Kiingereza na lugha ya Kiswahili ilikuwepo. Ukoloni umeathiri matumizi yetu ya lugha nchini Tanzania kwa sababu ya kutulazimisha kutumia lugha yao ya Kiingereza.

Tunaweza kuhakikisha lugha zote zinathaminiwa kwa kupata ujasiri wa kuongea na kupata haki ya kuongea kuhusu lugha zetu.

7

Mbeleni, nataka kuwa na gari na kujifunza kuendesha ili kutembelea sehemu mbalimbali kama Dar es Salaam, Monduli, na Kigoma.

Ninataka kuwa mwalimu ili kuwafundisha wanafunzi lugha nyingi kama Kiha, Kichaga, Kimaasai, Kiingereza, na Kifaransa nina hamu sana ya kujifunza. Nitawapa watoto mifano ya kutokata tamaa na lugha zao. Nitawaambia wajiwekee ndoto zao na vipaji vyao ili kuwasaidia wazazi, wanafunzi, watoto, na wazee.

Asante. Naas.

8

Ninaitwa Ester. Ninajua lugha 5: Kiingereza, Kiswahili, Kichaga, Kumbulu, Kifaransa. Kusalimia kwa Kifaransa ni Comment ca va. Kiingereza: Good morning. Kichaga: Kwamza mae, Naiyo mae. Kimbulu: Aidorii, Aidomaa. Kiswahili: Shikamoo, Marahaba.

Kichaga ninatumia nyumbani. Kiswahili hutumia kanisani, barabarani, shuleni, na kwingine. Ninatumia Kifaransa ninaposikia nyimbo, kwenye klabu, na nikisoma tableti. Ninatumia Kimbulu kwenye klabu.

9

Kiingereza natumia shuleni, nyumbani, nikisoma vitabu na tableti, hospitali, na jikoni.

Ninapenda Kiswahili kwa sababu ni lugha ya taifa langu la Tanzania. Pia ninapenda lugha yangu ya Kichaga kwa sababu mimi ni mzaliwa wa Uchagani. Owenyi ngafundishwa na bibi woko Kichaga.

Kichaga ni muhimu kwenye maisha yangu kwa sababu ni asili ya kabila langu. Hunikumbusha asili ya nyumbani. Nimejifunza lugha hiyo nilipokuwa kwa bibi mkoani Kilimanjaro.

10

Ninawafundisha Kichaga kidogo. Nikisema ninanawa mikono kwa Kichaga: Njikesamba maoko. Miguu inauma ni Marende yakewawa. Ninacheka ni Njikeseka.

Huko mbeleni nataka kujua Kipare kwa sababu mamangu ni mzaliwa wa huko Upareni. Nitajifunza lugha hiyo Upareni nikienda kwa babu yangu. Nitaomba nifundishwe na niweze kushika ili nao wawe na moyo wa kunifundisha.

Napenda kujua lugha nyingi kwa sababu nitazitumia nitakapokuwa rubani.

11

Ukoloni umeathiri lugha zetu kwa sababu walikataa tusifundishwe shuleni. Walitaka lugha yao ithaminiwe. Tunatakiwa kuthamini lugha zote shuleni, sio Kiswahili na Kiingereza tu.

Tuwe na umoja ili tuweze kuwaambia watu kuthamini lugha zote. Wakoloni waache ubabe wao wa kukataa tusiongee lugha zetu. Wanatakiwa wathamini lugha zetu na sisi tuthamini lugha zao. Wakoloni waache unyonyaji nchini Tanzania. Mimi ninaikataa.

12
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Lugha za Maisha Yetu
Author - Wasichana wa Shule ya Msingi ya Mwasi Kaskazini
Illustration - Klabu Ya Hadithi Zetu
Language - Kiswahili
Level - Longer paragraphs