Safari ya Kuja Montreal
Makusaro Shank Lauwo

Tulikuwa Mwasi kwetu.
Tulisubiri safari yetu ya kwenda Montreal kwa hamu.

1

Tulipanga mizigo yetu kwa ajili ya safari.
Mizigo ilikuwa sita.
Sisi tuliweka vitu vingi ndani ya mizigo yetu.

2

Asubuhi, tulipeleka mizigo yetu kwa Hube. Tuliacha mizigo mitano kwenye nyumba ya Hube ya zamani, na mzigo mmoja kwenye nyumba yake mpya karibu na Shule ya Mwasi Kaskazini.

3

Tulipanda bajaji ya Godi kwenda site.
Gari lilienda kuchukua mizigo yetu kwa Hube halafu gari likaja site kutuchukua.
Halafu tulienda uwanja wa ndege.

4

Tulipofika uwanja wa ndege, tuliweka mizigo yetu mikubwa chini ya ndege.
Halafu tulipanda ndege.

Ndege ilipaa saa moja. Tulipewa chakula.

5

Halafu tukapanda ndege nyingine Addis Ababa.
Halafu tukapewa chakula tena.
Mizigo yetu mikubwa ilihamishwa kutoka chini ya ndege, ikawekwa chini ya ndege ya pili.
Tulikaa kwenye ndege ya pili kwa muda mrefu.

6

Ndege ya pili ilitufikisha hadi Ufaransa.
Halafu tukapanda ndege ya tatu Ufaransa.
Mizigo ilihamishwa kutoka ndege ya pili kupelekwa hadi ndege ya tatu.

7

Tulipoingia ndani ya ndege na ndege ilipopaa, tulikula chakula.

Ndege ya tatu ilitufikisha hadi Montreal.

8

Tulipofika Montreal, mizigo yetu ikatolewa chini ya ndege.
Halafu tulienda kuichukua.

Halafu tulienda kupanda taxi. Taxi yetu ilitufikisha nyumbani 5427 Rue Hutchison.

9

Nilijisikia furaha kwa sababu tulikuwa tumefika Montreal.
Tuliona vitu vizuri, kwa mfano snow na sled.

10

Tulicheza na bibi na babu.
Halafu tukatengeneza train tracks na babu na bibi.

11
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Safari ya Kuja Montreal
Author - Makusaro Shank Lauwo
Illustration -
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs