

Hapo zamani za kale, paliondokea wanyama wawili. Mmoja aliitwa Punda na mwingine Sungura.
Punda na Sungura walikuwa marafiki wa chanda na pete. Walikuwa wanaishi katika nyumba tofauti.
Walikuwa wanasaidiana kufanya kazi zao za nyumbani kisha wakimaliza wanaenda kucheza na kupumzika pamoja.
Siku moja walipokuwa wakitembea sungura alimwambia punda, je unajua nyasi ni kijani kibichi punda alikataa na kusema kuwa nyasi ni nyekundu.
Sungura alisema basi twende kwa mfalme simba tumuulize na basi punda akakubali.Sungura akamkalia mgongoni kisha wakaenda kwa mfalme.
Walipofika kwa mfalme, mfalme alikubali kuwa nyasi ni nyekundu na akasema kuwa sungura atahukumiwa asiongee kwa mwaka mmoja punda alifurahi na kwenda akitabasamu.
Hata hivyo punda alivyoenda sungura alimuuliza simba kwanini umenihukumu. Simba akamwambia ni kwa sababu sungura ni mwerevu na anabishana na wanyama wajinga kama punda.

