Mazingira
Emanueli Blasidi Temba
Emanueli Blasidi Temba

Katika mazingira yetu kuna wanyama na atapia wadudu wa aina mbalimbali kama ampibia reptilia mamalia na wadudu wengine mbalimbali.

1

Mimi ninapenda kuchora. Uchoraji ni kipaji cha maisha yangu. Mimi nimechora ramani hii. Ni nzuri sana. Hutusaidia mahali popote pale katika maisha. Naamini nina kipaji kizuri sana cha kuchora. Kinanisaidia katika maisha.

2

Katika mazingira kuna wanyama na wadudu wa aina mbalimbali kama jogoo, sungura, ngombe na
wadudu ,kama nyoka sisimizi na nondo.

3

Kilimo ni kizuri katika mazingira kwasababu kilimo hutupatia chakula katika familia na hata jamii inayo tuzunguka.

4

Mazingira yetu watu wengine hawapendi kushiirikiana katika jamii yetu katika picha hii inaonesha watu wanavyo penda kushirikiana na wasioshirikiana katika mazingira kuna wanyama waaina mbalimbali kama nyani na nyoka.

5

Mimi ninajivunia kipaji hiki cha kuchora kwasababu ni kizuri sana na ninapenda uchoraji ni mzuri sana na ninapenda kuchora sana marafiki zangu ,wengi wanajua kuandika kusoma na kuchora.

6

Wanyama hawa wengine huhishi mistuni katika mazingira yao wanaoishina pia wengine tunaoishi nao katika jamii na katika mazingira tunaeyoishi kila siku na wanyama hao ni pamoja na mbwa ngombe mbuzi kondoonawanyama wengine mbalimbali.

7

Watu wanapenda kuwa na gorofa nzuri sana katika majengo na katika jamii yetu. Ndivyo watu hupenda hivyo sana kwa sababu ni nzuri.

8

Gari ni aina ya chombo cha usafiri ambacho hutumika na binadamu katika usafiri wa aina mbalimbali katika jamii.

9

Fuso ni aina ya gari linalobeba mchanga, matofali, mawe, na simenti na hufanya kazi nyingine mbalimbali.

10
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Mazingira
Author - Emanueli Blasidi Temba
Illustration - Emanueli Blasidi Temba,
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs