

Mimi ninaitwa Ismail. Ninasoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Mazoezi.
Ninapenda kusoma vitabu mbalimbali, kwa mfano vitabu vya hadithi mbalimbali. Ninapenda kusoma vitabu ili kutimiza ndoto zangu za baadaye.
Watu ambao ni muhimu kwenye maisha yangu ni mama yangu na baba yangu kwa sababu wao ndio walionilea mpaka nimefikia hapa nina miaka 12. Na ninasoma darasa la 6.
Sehemu zenye umuhimu kwenye maisha yangu ni maktaba, shuleni na nyumbani kwetu. Maktaba ni muhimu kwenye maisha yangu kwa sababu inanifunza vitu vingi.
Shuleni pia ni sehemu muhimu kwenye maisha yangu kwa sababu shuleni patanisaidia kufikia malengo yangu ya baadaye. Nyumbani pia ni sehemu muhimu kwa sababu ndipo ninapoishi.
Kitu kilichotokea kwenye maisha yangu na kuacha alama ni kukaa mbali na ndugu zangu na mamangu. Mimi nilikaa mbali na ndugu zangu na mama yangu kwa sababu nilienda Zanzibar kwa baba yangu kwa muda wa miaka 3.
Nilienda Zanzibar kumsalimia baba yangu na nikasomea huko. Maisha ya Zanzibar nilikuwa sijayazoea. Nikamwambia baba yangu nimemkumbuka mama yangu.
Baba yangu alipo kuwa anaenda kazini nilikuwa napenda kuangalia ndege na elkopter na vingi nevyo.
Nikamwambia baba mimi ninataka kuenda kwa mama. Nikarudi huku Monduli kwa mama yangu.
Ninamshukuru mungu kwa kuendelea kunipa uzima na kuendelea kuja maktaba kujifunza vitu vingi hadi kufaulu katika masomo yangu.
Pia ninamshukuru mungu kwa kunipa pumzi kwenye maisha yangu na kunileta duniani pamoja na wazazi wangu. Na kunipa nafasi ya kuishi na mama yangu na ndugu zangu huku Monduli.
Kitu nilichowahi kufanya chenye mafanikio kwenye maisha yangu ni kufaulu mtihani wa taifa wa darasa la 4 na kuleta mafanikio katika jamii yangu.
Niliwahi kufanya vizuri katika masomo ya darasani na kuleta mafanikio katika jamii yangu. Mama yangu na ndugu zangu walinipa hongera. Mpaka leo mama yangu ananiambia niende shule nikasome kwa bidii ili kutimiza ndoto zangu.

