

Katika Kijiji cha tupendane kulikuwa Na vijana wawili Na walipendana kama Chanda Na pete kwasababu walikuwa majirani.
Vijana walikuwa ni Katana Na Kahindi nawalipenda Sana kucheza Mpira wakandanda na walipenda kufanya kazi haraka ili wapate muda wakucheza.
Siku moja Katana alitumwa na mama yake Kuenda dukani kununua Nyanya, Karoti,vitunguu Na vinginevyo.Katana alichukua tufe la Mpira ambalo alienda na kucheza njiani
Alivyokuwa akikimbia njiani huku akicheza kwa bahati mbaya pesa zikapotea.katana alirudi nyuma Huku akitafuta pesa mbele yake alikutana na rafiki mmoja mjanja Sana na Katana alishuku kuwa ameziokota hizo pesa.
Katana alichukua hatua ya kumkimbilia rafiki mjanja .Kwa Bahati nzuri Yule rafiki yake alikuwa ameziokota na akamregeshea Katana .
Katana alimshukuru rafiki mjanja Sana . Katana alikimbi dukani kununua vitu alivyo kuwa ametumwa na mama yake.
Na alivyorudi nyumbani mama yake alimwongelea Na kumwambia wasicheze Mpira tena njiani. Kila jumamosi atampa nafasi ya kucheza na marafiki sake.

