Mwanabiashara maarufu
JUDY J KADZO
Catherine Groenewald

Hapo Zamani paliondokea mwanabiashara mdogo aliyeitwa Miyamoto. Kijana Huyu alikua akiuza Mboga Na matunda kutoka Katika shamba lake.Alikua akilima yeye na familia yake.

1

Aliendelea kufanya Biashara Na kuwekeza polepole. Baada ya miaka mitatu alikua ana pesa shillingi 692000.

2

Miyamoto aliamua kutafuta ushauri kwa mzee Sifa.Mzee alimwambia atumie pesa hizo kujenga duka Na kuleta bidhaa zinazohitajika wanakijiji.

3

Baada ya yote kuyafanya alikua maarufu.

Aliwahudumia wateja wake bila kubagua. Alifungua duka la kuuza nafaka. Pia aliendelea Na ukulima wake.

4

Biashara ilivyozidi kukua Miyamoto aliwaajiri vijana na kulipa Ada ya serikali ya kaunti bila kukoma.

5

Baada ya miezi michache, Baadaye Jina Lake lilibadilika Na kuwa mwanabiashara hodari .Hayo Yote yalitokea kupitia kwa juhudi zake

6
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Mwanabiashara maarufu
Author - JUDY J KADZO
Illustration - Catherine Groenewald
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs