Siku ya soko
Leon mramba Emmanuel baraka

Kila jumanne Huwa ni siku ya soko kwetu. Soko Huwa hufanyika matanomanne .Huwa kunauzwa viatu vingi.

1

Jumanne iliyopitailikuwa siku ya furaha sana kwasababu tulipewa pesa na mjomba. Mimi na rafiki yangu tulienda huko sokoni. Tulienda huko ili tununue nguo za Christmas. Kila mmoja wetu alikuwa na pesa za kutosha.

2

Tulikuwa na elfu mbili za kutumia. Tulipanga kununua nguo na viatu. Christmas hii tulipanga tutangara sana na nguo mpya.

3

Tulienda kununua nguo zilizo itwa 2face na anguka nayo nguo hizo zilikuwa ndizo fasheni huo mwaka huo.Kila mmoja uliye muona alikuwa amenunua nguo hiyo.

4

Tulipomaliza kununua nguo pesa zilikuwa zimeisha. Nguo zetu zilikuwa zinauzwa pesa Gali kwa hivyo hatukuweza kununua viatu. Tuliamua tuta nunua viatu tukipata pesa zengine.

5

Tulipokuwa tunatoka hapo sokoni tulimuona shangazi wangu alitupa shilingi hamsini tugawanye. Tuligawanya tukanunua viazi na barafu. Wakati tulipokuwa tunakuja nyumbani hatukuchukuwa bodaboda.

6

Tulienda nyumbani kwa miguu . Nilipofika nyumbani kulikuwa tayari jua limezama . Mama yangu alinichapa sana . Alinichapa kwa sababu nilikuwa nimechelewa kurudi nyumbani na alidhani nilikua nikicheza na marafiki.

7

Mamangu alikasirika sana nilikuwa sikufanya kazi za nyumbani .Aliniambia kwamba hataninunulia viatu vya Christmas. Nilibaki na huzuni na kilio.Niliamua Nita vaa viatu vyangu vya shule Christmas

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Siku ya soko
Author - Leon mramba Emmanuel baraka
Illustration - , Rob Owen
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs