

Kijiji chetu kinaitwa Gotani. Kiko karibu na msitu mkubwa.
Gotani kuna wakulima hodari waliokomaa kama mama yangu.
Katika msitu huo ulio karibu, kuna ndovu mmoja mweusi.
Ndovu huyo amekuwa msumbufu kijijini kwa miaka miwili.
Wanakijiji waliamua kuchukua hatua kupeleka ripoti kuhusu usumbufu wa ndovu huyo.
Maafisa wa kutunza wanyamapori hawakuchukuwa hatua yoyote kuhusu ndovu huyo mharibifu.
Usiku mmoja, ndovu huyo aliingia shambani kwetu.
Aliharibu mihogo yetu iliyokuwa karibu kuvunwa.
Usiku huo alikula mimea yote shambani.
Asubuhi ilipofika, mimi na mama yangu tulienda shambani. Tuliona mihogo yetu imetapakaa shambani.
Mama alibaki mdomo wazi na mwenye huzuni mwingi.
Mama aliwaza jinsi angekadiria hasara aliyokuwa amepata. Biashara yake ilikuwa imeharibiwa.
Mama alikuwa mkulima na mfanya biashara maarufu sana wa mihogo kijijini kwetu.
Baada ya wiki moja, mama na baba waliamua Kumuua ndovu huyo. Walitengeneza mtego ambao ungemdhuru ndovu huyo.
Mtego huo ungemdunga tumboni. Sumu ingeenea miwilini na kusababisha kifo chake.
Maafisa wa kutunza wanyamapori walipopata habari hizo, waliamua kumrudisha ndovu huyo kwenye Mbuga ya Wanyama.
Kijiji chetu cha Gotani kiliishi kwa amani.

