Mashairi ya Kipekee
Eliza Njau
Shule Ya Msingi Mwasi Kaskazini

NDOTO ZETU

Tuna ndoto za maisha, tusikatishwe tamaa,
Tuwezeshwe tunaweza, watoto tunatakiwa,
Tusikilize sanaa, watoto wote jamaa,
Ndoto nyingi za watoto, jamani zisikilizwe.

Tusikate tamaa, tuwezeshwe na tuweze,
Tuna haki nyingi sana, jamani tusikilizwe,
Watoto tunaweza, jamii ituwezeshe,
Ndoto nyingi za watoto, jamani zisikilizwe.

1

Msiwafanye watoto kuwa yaya wa nyumbani,
Wakati wana ndoto nyingi za maishani,
Ndoto za faida nyingi, tuna ndoto nyingi jamani,
Ndoto nyingi za watoto, jamani zisikilizwe.

Baba na mama, muendeleze ndoto
Tusije tukakwamishwa, watoto wana ndoto zao.
Wakati wanazikuza, tutoe taifa lao
Ndoto nyingi za watoto, jamani zisikilizwe.

2

Asanteni wazazi, kuendeleza hizi ndoto
Kama si nyinyi walezi tusingeweza kufika hapa.
Ndugu, jamaa, na marafiki, mtufundishe hayo.
Ndoto nyingi za watoto, jamani zisikilizwe.

3

BIASHARA NI MUHIMU

Watu tuna biashara, nyingi maishani mwetu,
Maduka ni biashara, maisha haya yetu,
Zisikatazwe tena, watu wengi huja kwetu,
Biashara ni muhimu, kwenye maisha ya watu.

Hata wa hotelini, fanyeni kazi vizuri,
Jamii hii jamani, jamani tuwezeshweni,
Kufika hapo jamani, sio mbali jamii,
Biashara ni muhimum, kwenye maisha ya watu.

4

Tuwezeshwe na tuweze, biashara vibandani,
Jamii ituwezeshe, sio kuteswa nyumbani,
Jamani tusaidiwe, tena na tena jamii,
Biashara ni muhimu, kwenye maisha ya watu.

Tupate na ajira, huko viwandani,
Tusije tukakwamishwa, vikwazo sikwamisheni,
Watu hawa jamaa, biashara kwetu sisi,
Biashara ni muhimu, kwenye maisha ya watu.

5

Tushughulike nayo, tusiacheni hayo,
Yatusaidiayo, tusiache hayo,
Jamii ya kwao wao, iendeleze hayo,
Biashara ni muhimu, kwenye maisha ya watu.

6

SHAIRI LA KUHUSU WATOTO

Watoto wetu jamani, msiache kwenda shuleni,
Huko kwa faida nyingi, kuliko kukaa nyumbani,
Hakuna faida nyingi, ukikaa nyumbani,
Epukeni hizo mimba, jamani za utotoni.

Tuwashukuru wazazi, kuwasomesha watoto,
Kuwafundisha vizuri, huko madarasani kwao,
Walimu tuwashukuruni, kuwasomesha watoto,
Epukeni hizo mimba, jamani za utotoni.

7

Hadi mbali wamefika, kama si nyinyi walimu,
Tusingeweza kufika, na hawa wazazi wetu,
Twawashukuru sana, kwa kutufundisha walimu,
Epukeni hizo mimba, jamani za utotoni.

Tusome kwa bidii, tufikie malengo,
Tuliyojiwekea jamani, hiyo si kazi ndogo,
Bila kusoma vizuri, hatuwezi fika hapo,
Epukeni hizo mimba, jamani za utotoni.

8

Watoto tuacheni, hizo tabia mbaya,
Zisizopendezeni, kwa jamii kwa ujumla,
Someni hivyo vitini, ili kupata maarifa,
Epukeni hizo mimba, jamani za utotoni.

9

KILIMO

Wote husisha kilimo, kwa jamii ielewe,
Umuhimu wa kilimo, yatupasa tuelewe,
Mbogamboga ni kilimo, familia tuelewe,
Umuhimu wa kilimo, sisi sote yatuhusu.

Bustani za mbogamboga, nayo pia ni kilimo,
Nazo pia kuzipanga, ni msingi wa kilimo,
Tuyaepuke majanga, kulima na kilimo,
Umuhimu wa kilimo, sisi sote yatuhusu.

10

Tupewe pia elimu, ya kuhusisha kilimo,
Twahusiwa na walimu, kuhusu pia kilimo,
Tujipatie elimu, kumwagilia kilimo,
Umuhimu wa kilimo, sisi sote yatuhusu.

Pia umwagiliaji, sisi sote kwa jamii,
Mbolea huhitaji, ni muhimu maji,
Kilimo kinahitaji, kilimo na ufugaji,
Umuhimu wa kilimo, sisi sote yatuhusu.

11

Kalamu naweka chini, tamati nimefika,
Hatukuwa hatarini, na hata hiyo nafaka,
Ninamaliza mwishoni, sasa tumeelimika,
Umuhimu wa kilimo, sisi sote yatuhusu.

12

UFUGAJI

Jamani ufugaji, huleta mapato,
Kwa watu na wafugaji, huwasaidia wao,
Tusiache ufugaji, huo ndio utusaidiao,
Jamani ufugaji, huleta ajira nyingi.

Kuna msemo usemao, kujaribu kushindwa,
Na kweli majaribio, sio kushindwa kabisa,
Jamani wanyama hao, hutakiwa kunenepa,
Jamani ufugaji, huleta ajira nyingi.

13

Hao wanatakiwa, kula vitu muhimu,
Kama vile chakula, kwa mifugo ni muhimu,
Kwa jamii ya sasa, huwasaidia watu,
Jamani ufugaji, huleta ajira nyingi.

Wanatakiwa kula, chakula cha majani,
Kwa wale wanyama, wanaokula majani.
Tusiwakatishe tamaa, hawa wafugaji,
Jamani ufugaji, huleta ajira nyingi.

14

Kupata ajira zao, kama vile vipato,
Huko maishani mwao, ufugaji muhimu kwao,
Una faida nyingi zao, kuleta mapato yao,
Jamani ufugaji, huleta ajira nyingi.

15

VIPAJI VYETU

Watoto tuna vipaji, vingi maishani mwetu,
Wazazi fundisheni, kwa watoto wenu,
Sio kazi rahisi, kwa wazazi wetu,
Vipaji vya faida nyingi, pia huleta ujuzi.

Jamii itufundishe, na kuendeleza vipaji,
Kwani za faida nyingi, za kukuza vipaji,
Fundisheni hayo yote, yakuzayo vipaji,
Vipaji vya faida nyingi, pia huleta ujuzi.

16

Ili tusije kwama, kwa vikwazo vya wengine,
Visije kuleta shida, kwa watu na wengine,
Ili tusije pata, hivi vikwazo vingine,
Vipaji vya faida nyingi, pia huleta ujuzi.

Pia huleta hasa, kwa jamii kwa ujumla,
Tusije tukakwamishwa, hivi vipaji jamaa,
Na visije vikakwamisha, hasara hutupata,
Vipaji vya faida nyingi, pia huleta ujuzi.

17

Na kuleta matatizo, hiyo ni shida kubwa,
Kwa vipaji vya watu hao, huleta hasara kubwa,
Kwa watu na mali zao, tusikate tamaa,
Vipaji vya faida nyingi, pia huleta ujuzi.

18

LUGHA ZETU

Tuwafundishe watoto, lugha nyingi maishani,
Tuwafundishe watoto, lugha tena maishani,
Waweze kujua hayo, watoto na lugha nyingi,
Lugha ni muhimu sana, kwa makabila yote.

Tufundishane lugha, mbali za makabila,
Ili tuweze kujua, kwa watu hawa wakubwa,
Watufundishe lugha, kwa wakubwa na wadogo,
Lugha ni muhimu sana, kwa makabila yote.

19

Katika jamii yetu, ili tuweze kujua,
Hizi lugha za kwetu, na kujifunza haya,
Lugha ni muhimu kwetu, kwa jamii kwa ujumla,
Lugha ni muhimu sana, kwa makabila yote.

Tuweze kufundishwa, hizi lugha mbalimbali,
Na jamii kwa ujumla, kwa makabila mengi,
Sisi tusiyoyajua, kufundishwa lugha hizi,
Lugha ni muhimu sana, kwa makabila yote.

20

Tujue lugha nyingi, tunazofundishwa maishani,
Wazazi na walezi, tufundishane jamani,
Ili tuweze jueni, hizi lugha maishani,
Lugha ni muhimu sana, kwa makabila yote.

21
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Mashairi ya Kipekee
Author - Eliza Njau
Illustration - Shule Ya Msingi Mwasi Kaskazini
Language - Kiswahili
Level - Read aloud