

Ninaitwa Olimpya. Ninasoma darasa la sita katika Shule ya Mwasi Kaskazini. Nina miaka kumi na moja. Ninaishi na wazazi wangu. Watu wenye umuhimu katika maisha yangu ni Mungu, baba, mama na marafiki.
Sehemu zenye umuhimu maishani mwangu ni kanisani kwa sababu ninaenda kusali, shuleni ninapoenda kutafuta elimu, na nyumbani kwa sababu ninapata kila kitu kama vile mavazi, malazi, na mahitaji yote ya shule.
Nyumbani ninafanya kazi za aina za kuosha vyombo, kudeki, kufagia, kuchota maji, kuzoa mbolea, na kufua. Nina kipaji cha kuchekesha watu.
Najivunia kwa kuwa nakaa na ndugu wote kama vile babu na bibi. Namshukuru Mungu wangu kwa sababu ndiye aliyenipa uhai wa hapa duniani na mpaka sasa ninaishi. Kama siyo yeye sijui ingekuwaje.
Napenda kuuza duka baadaye nitakapokuwa mkubwa kwa sababu hunipatia kipato. Pia ninaweza kuwasaidia wazazi wangu baadaye. Napenda kuuza duka langu ili niwasaidie wajane, yatima, wagonjwa, na maskini.
Ninawapenda sana wazazi wangu kwa moyo wangu wote. Nitawajengea wazazi wangu nyumba. Namuomba Mungu ewe nami daima.

